Mradi huo utahusisha uboreshaji wa Barabara, Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.
Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.
Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.
Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kufungua miradi itakayowaingizia kipato.
Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.
Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.
Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
Post a Comment