Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC MAKONDA ATOA NEEMA YA UPIMAJI AFYA BURE KWA WANANCHI DAR ES SALAAM

69b6c4c8-8321-4401-8bbd-e51c2441e7bf (1)
Miongoni mwa watu wetu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na matatizo mbalimbali katika miili yao bila kujua hasa nini chanzo.

Hata hivyo wengi wao pia hupenda kujua nini kinachowasumbumbuwa lakini uwezo wa kifedha kuwa mdogo wakati mwingine umekuwa ni chanzo kikubwa kwao hasa inapofikia muda wa   kupata  huduma za vipimo  sahihi hospitalini.
 

Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam imetoa siku 5  kwa wananchi wa Mkoa wa Huo kujitokeza siku ya jumatano tarehe 6 Septemba mwaka huu  katika viwanja mnazi mmoja ,kupima afya zao.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ambapo amesema serikali yake imeona ni vyema kuendeleza huduma ya afya, hivyo wananchi wote wa mkoa huo wametakiwa kujitokeza kuanzia asubuhi mpaka jioni kupima ili kujua afya zao.

“Kitendo cha kupima afya kinatoa unafuu wa kujua namna gani ya kujipanga katika sekta nzima ya afya ilikupunguza vifo,kuna magonjwa mengine ambayo huwezi kuyafahamu mpaka upimwe alafu ugundulike kinachokusumbua,na wakati mwengine ukichelewa kupatiwa huduma, huwapa shida kubwa madaktari na hata wewe mwenyewe unaweza kupoteza maisha yako kwa kuchelewa kujua kinachokusumbua”Alisema Makonda.

Ameleeza kitendo hiki kinamhamasisha mwananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya ambapo kufanya hivyo kunarahisisha kuepusha gharama, na kuondokana na Magonjwa ambayo ungeweza kuyaepuka endapo utapata taarifa mapema.

Magonjwa yatakayopumwa ni pamoja na kansa,tezi dume,macho,meno,na kila aina ya ugonjwa .
Aidha Makonda amesema kutokana na changamoto ya ugonjwa wa homa ya ini , madaktari wanajipanga kuona namna gani wanaweza kushughulika na ugonjwa huo.

Amefafanua kuwa lengo lake ni kuona hakuna mwananchi ambao watakufa kwa kukosa huduma ya afya isipokuwa mgonjwa afe kwa mapenzi ya Mungu.

Upimaji huo utakuwa ni bure bila tozo ya aina yeyote,ambapo wataalamu zaiidi ya mia mbili watakuwa tayari kwa kutoa huduma kwa wananchi  watakao jitokeza.

Nae Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Grace Magembe amesema zoezi hilo limeshirikisha wadau kutoka serikalini na wengine wa taasisi binafsi ambapo kwa upande wa Serikali, madktari kutoka hospitai ya Taifa Muhimbili Jakaya Kikwete, Ocean Road, Amana, Mwananyamala, Temeke, wengine ni TMJ, LEGENCY, AGAKHAN, IMILIFE, Chama cha watoa huduma binafsi, CCP MEDICINE, DAMU SALAMA, Shirikaa la MDH, Shirika la bima ya afya NHIF, KAIRUKI, SANITAS.N.K

Amesema wagonjwa wote watahudumiwa na wale watakao stahili kupata rufaa atapewa kuwakati unaotakiwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top