Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Dodoma unapenda kuwajulisha Vijana wake Mkoani Dodoma mnamo Tarehe SEPTEMBER 7.Mwaka 2017 Saa 3:00 Asbh katika Ukumbi wa NEC (White House) kutakuwa na Uzinduzi wa Programme Maalum ya Ushiriki wa Vijana wa CCM katika Miradi ya Maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Progaramu hii imelenga kuwajengea uwezo na maarifa kwa Vijana wa CCM kujiamini hatimaye kuzitumia fursa na ushiriki wao wa moja kwa moja katika shughuli za Serikali , miradi ya Maendeleo ikiwemo ile ya Kiuchumi na Kijamii.
Msingi wa Programu hii ni kuawapa nafasi Vijana wa CCM ya kuwa wadau wakuu na wa kwanza katika ufanikishaji wa shughuli za Kiuchumi na Kijamii jambo ambalo litaleta chachu na hamasa ya Vijana na ushiriki wa moja kwa moja.
Mgeni rasmi katika siku ya Uzinduzi ni ND. SHAKA .H. SHAKA (Kaimu Katibu Mkuu Wa UVCCM TAIFA )
Hivyo wewe kijana upatapo taarifa hii mjulishe na mwenzako bila kusahau.
Kwa wale watakaohudhuria hafla hiyo tuzingatie kuvaa sale za Chama.
*Kidumu Chama Cha Mapinduzi*
WOTE MNAKALIBISHWA.
Post a Comment