Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, ameibuka na kukana tuhuma zilizotolewa na mzazi mwenzake Faiza Ally aliyedai Sugu amemtelekeza mtoto wake aitwaye Sasha.
Faiza alitumia ukurasa wake wa Instagram kutoa malalamiko yake kwamba Sugu hatoi ada, chakula na malazi kwa mtoto wao.
Sugu ametumia risiti za benki alizolipia ada ya mtoto wake Mei mwaka huu, kama ushahidi alioutoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuonyesha kwamba amekuwa akitekeleza majukumu yake kama baba.
“Huwa sipendi kuposti mambo haya ila imenibidi hizi ni risiti za ada ya mwisho niliyolipa kwenye shule ya awali (Kindetgaten) , aliyokuwa anasoma mwanangu za mwezi wa tano mwaka huu ambako alishamaliza,” aliandika Sugu.
Alisema mwezi huu alitakiwa kuanzisha shule ya awali Feza iliyopo Mikocheni, lakini ghafla alipigiwa simu na mama mtoto wake huyo na kuzuiwa kumuona mtoto.
“Ghafla akanizuia na kusema hahitaji tena nilipe ada na hata nisimuone tena Sasha na ana uwezo wa kumpeleka huko Hazina International ambako pia hata hivyo nilishaanza kuwasiliana na uongozi ili niendelee tu kulipa ada hata kama nimepigwa marufuku kumuona mwanangu bila sababu,” alisema na kuongeza;
“Hivi kama ni nyie mngefanyaje? Na nyie mnaotukana ovyo mitandaoni bila kuwa na ukweli mnaoujua tafadhali sana naomba hebu kwanza kabilianeni na hali zenu kwenye maisha.”
Loading...
Post a Comment