Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tamko la Serikali kuhusu matibabu ya Lissu

Serikali imesema ipo tayari kugharamia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo familia itaomba jambo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , na kusema kwamba kama familia itahitaji na ripoti ya madaktari ikionyesha kuna ulazima wa Tundu Lissu kupatiwa matibabu zaidi, serikali itasimamia suala hilo.

Hivi karibuni kumekuwa kukiendeshwa kampeni ya kuchangia matibabu ya Tundu Lissu baada ya gharama zake za matibabu kuwa kubwa huku baadhi ya watu wakiitupia lawama serikali kwa kushindwa kusimamia hilo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top