Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanzania yaikana vikali Korea Kaskazini

Serikali imekanusha vikali taarifa kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ina mahusiano ya kibiashara na Korea Kaskazini ambayo imewekewa vikwazo vya kiuchumi na baraza hilo.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema kuwa licha ya uhusiano uliokuwepo awali, lakini tangu mwaka 2014, Tanzania imepunguza uhusiano wa kibiashara na kidiplomasia na nchi hiyo.

“Hatuna ugomvi na Korea Kaskazini, lakini kwa mpango wake wa kutengeneza makombora ya masafa marefu ya nyuklia sio mzuri kwa heshima na usalama wa duniani, ndiyo maana tukaanza kuchukua hatua za kupunguza mahusiano.” alisema Dkt.Mahiga

Aidha, Dkt. Mahiga aliongeza kuwa uhusiano huo wa kibiashara ulikuwepo kabla ya vikwazo vilivyowekwa hivi karibuni na Baraza la Umoja wa Mataifa

Tanzania na Uganda ni miongoni mwa baadhi ya nchi zinazochunguzwa na Umoja wa Mataifa kwa tuhuma za kwenda kinyume na vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.

Ripoti ya uchunguzi huo ilitolewa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa tarehe 9 mwezi wa Septemba. Baraza la Usalama la Umoja ikisema linachunguza tuhuma za Tanzania kuingia mikataba ya kijeshi na Korea Kaskazini inayogharimu dola za kimarekani milioni 12.5
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top