JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani wamewakamata watuhumiwa wawili ambao wameshikwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Bhangi magunia nane.
Watuhumiwa hao walionaswa na Jeshi la Polisi wamefahamika kwa mjina Abraham Michael mwenye umri wa miaka 31 mkaazi wa Jijini Dar es Salaam na Godfrey Malakasuka mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa Kimara waliokamatwa katika eneo la Ubena Zomozi wakitokea Mkoani Morogoro kuelekea Jijini Dar es Salamaa.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Mkoa wa Pwani ACP Jonathan Shanna alisema kuwa watuhumiwa wamekamatwa na vidhibiti hivyo wanastahili kupata adhabu kali pindi watakapofikishwa mahakamani.
Post a Comment