Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri afunga Machimbo

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina amefunga machimbo ya mchanga katika kijiji cha Kolangwa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina.
Waziri Mpina amefikia uamuzi huo Septemba 21 kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimbaji wa mchanga katika machimbo hayo.

Mpina ametoa agizo la kufungwa kwa machimbo hayo akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa mazingira mkoani Pwani ambapo amebaini uharibifu huo umechangiwa na Taasisi za Serikali ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Idara ya Madini na Baraza la Taifa na Usimamizi wa Mazingira NEMC.

Waziri amebaini kuwa uchimbaji huo umefanyika bila wananchi kushirikishwa na haukuzingatia miundombinu na sheria ya Mazingira pia makazi ya watu.

Kufuatia mapungufu hayo, Mpina ameagiza Taasisi hizo za Serikali kufuatilia uharibifu huo uliofanywa kwa muda wa wiki mbili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top