Wavamizi hao wameanzisha mgodi usio rasimi katika shamba hilo.
Akizungumza na Nipashe shambani hapo jana, Buholo alisema anamiliki shamba hilo tangu mwaka 2004 na kwamba alinunua kwa ajili ya shughuli ya kilmo bila kufahamu kama kuna madini ya dhahabu ardhini.
Nipashe ilijionea makundi makubwa ya wachimbaji wadogo wakiwa katika pilika ya uchimbaji wa dhahabu shambani humo.
Buholo alisema "majuzi" wakati akipalilia mahindi kwenye shamba hilo aliokota jiwe lenye madini ya dhahabu, na kwamba baada ya kulichakata alipata dhahabu yenye "uzito wa pointi saba."
Alisema alipouza dhahabu hiyo na taarifa kufikia watu wengine, ndipo wachimbaji walivamia eneo hilo na kuanzisha uchimbaji wa madini hayo.
Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Lwangasa Lumumba Salvatory Musogera amesema kugundulika kwa dhahabu shambani humo si mara ya kwanza katika kijiji hicho.
Post a Comment