Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli Atangaza Kiama kwa Wakuu wa Mikoa

Rais  Dk. John Magufuli amesema   mkuu wa mkoa yoyote atakayeshindwa kupeleka wawekezaji   kujenga viwanda katika mkoa wake hatamvumilia.

Amewataka wakuu wote wa mikoa kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, ambaye amekaribisha wawekezaji wanaojenga viwanda vipya.

Agizo hilo alilitoa Mwanza jana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara eneo la Nyakato wilayani Ilemela.

Rais alisema viwanda si mali yake bali ni  mali ya wananchi ambao ndiyo walipa kodi.

Alisema ingawa Tanzania ilikuwa na viwanda vingi, hivi  sasa Watanzania wamebaki hawapati majibu vilikwenda wapi  hali inayoifanya Serikali  iamue kufanya kazi ya kuvifufua vya zamani na kujenga vipya.

Kabla ya kuhutubia mkutano huo Rais  alizindua kiwanda cha vinywaji baridi cha Sayona   kilichojengwa   Nyakato.  Leo anatarajiwa kuzindua viwanda vingine viwili.

Alisema amefurahishwa na ahadi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na kwamba kila anapopita ndani ya mkoa huo, lazima huzindua kiwanda ama viwanda kwa vile  wawekezaji wengi hukimbilia kuwekeza mkoani humo.

“Nataka nichukue fursa hii kukupongeza mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kuwatafuta wawekezaji wengi na kuwekeza kwenye viwanda.

“Nataka wakuu wa mikoa wa aina hii, mkuu wa mkoa ambaye kila siku napita mkoa wake bila kuzindua kiwanda sitamvumilia kufanya naye kazi, lazima ang’oke.

“Mkuu wa Mkoa ambaye haleti wawekezaji katika mkoa wake kujenga viwanda… kwanza hivyo viwanda si vya wakuu wa mikoa bali ni mali ya wananchi.  Kuwapo  viwanda kutasaidia kutengeneza ajira, hayo ndiyo maendeleo tunayotaka.

“Haiwezekani Tanzania iwauzie … tulime pamba tuwauzie wazungu watengeneze nguo  wazivae kisha kutuletea zikiwa mitumba.

“Tunataka  nguo zitengenezwe hapa na Mwatex ili ziuzwe kwa bei nafuu kuliko hiyo mitumba.  Sizuii mitumba lakini nguo mpya na bora lazima zitengenezwe hapa,” alisema Rais Magufuli.

Alimweleza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,  ajirekebisha na afanye kazi ya kufufua, kufunga na kuchukua viwanda visivyofanya kazi na   awape watu wengine.

“Haiwezekani unapewa kiwanda kutoka mwaka wa kwanza hadi wa 20 bila uzalishaji, wenye viwanda hivyo virudisheni haraka kwa sababu  tutakapoanza kuwashika tutadai faida ambayo walikuwa wakiipata miaka hiyo,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top