Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC MAKONDA ATOA GENERATOR, MABATI NA MIPIRA KWA CHAMA CHA MPIRA WA KIKAPU DAR








Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* leo ametoa msaada wa *Generator* ya kisasa, *Mabati 150* na *Mipira 110* kwa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam ili kujengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.

Generator hiyo ya kisasa ina uwezo wa *KV 35* na haitoi mngurumo wa sauti (silent) ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.*

*RC MAKONDA* amesema anataka kuona *Timu ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa* itakayotoa Wachezaji wakubwa wanaocheza *ligi za ndani na Nje ya Nchi.*

Uamuzi wa *RC MAKONDA* kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa Kikapu Uwanja wa Taifa na kujionea *Uchakavu wa Bati unaosababisha Wachezaji kunyeshewa na Mvua, Ukosefu wa Generator umeme ukikatika na uhaba wa Mipira* hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.

Aidha *MAKONDA* aliahidi kujenga *viwanja vitatu vya Mchezo wa Kikapu* ambapo tayari ramani imetengenezwa na *muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa Viwanja hivyo.*

Ili kuendelea kuimarisha Michezo Dar es salaam *RC MAKONDA* anaunda kamati maalumu ya kushughulikia michezo ya aina zote.

Tayari *RC MAKONDA* amepata mdau atakaejenga *Swimming pool* la kisasa Kinondoni kwaajili ya *Mchezo wa Kuogelea.*

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam *OKARE EMESU* amemshukuru *RC MAKONDA* kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top