Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shaka aanika siri ya Vijana wanaojiunga CCM toka upinzani



*ALIYOYASEMA KAIMU KATIBU MKUU SHAKA HAMDU SHAKA(MNEC) WAKATI AKIHOJIWA KUHUSU VIJANA WANAOTOKA UPINZANI NA KUJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI  IJUMAA 27 OKTOBA 2017 UPANGA DAR ES SALAM*

"Vijana watakaorudi na wanaondelea kurudi ndani ya Chama Cha Mapinduzi hawatabaguliwa, kutengwa wala kubughudhiwa badala yake watapata  haki zote za kikatiba pia kuthaminiwa kwasababu kila mwenda tezi na umo marejeo huwa ngamani" - Shaka

"Huu si wakati tena wa vijana kuwa nje ya  Chama cha Mapinduzi kwasababu vijana ndiyo wanaohitajika kurithi na kubeba  mikoba ya wazee na waasisi wanaostaafu."- Shaka

"Wakati umefika kwa vijana ambao aidha  kwa bahati mbaya au kwa kusukumwa na hamaki za kishabiki wakajikuta wanajiunga na upinzani hivyo huu ni wakati wao kurejea nyumbani" - Shaka

"CCM na jumuiya zake hazina vinyongo na wale wote waliojitoa kwa njia moja au nyingine kwani ccm ndicho chama pekee mlezi wa vijana hivyo kurudi kwao ndani ya chama si mkosi wala msiba" - Shaka

"Nimepokea maombi ya makundi ya vijana wanaotaka kurudi CCM tumewaelekeza waende wakapokelewe wilayani na mikoani kwao tunajua kila aendae tezi na umo marejeo huwa ngamani, CCM ndiyo baba na mama mlezi wa wana" - Shaka

"Vijana wenzetu rudini  kundini nje ya ccm ni kupoteza wakati bure hakuna  matarajio ya ccm kuondoka madarakani kwani hiyo ni ndoto isioaminika " -Shaka

"Serikali ya CCM sasa imekuwa ni ajenda,  gumzo, mijadala na somo kwa wasomi kwenye vyuo vikuu mbalimbali  afrika na mabara mengine wakiitisha makongamano kuzumgumzia ufanisi na utendaji wa serikali ya Rais Dk John Pombe Magufuli" - Shaka

" UVCCM ina taarifa za uhakika kuwa licha ya kurejea ccm aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro Fredrick Mushi lipo kundi kubwa la vijana wameamua kuukimbia upinzani na watarudi CCM muda si mrefu" - Shaka

"Atakayerudi tutampokea kwa mikono miwili ili aungane na timu ya ushindi, kikosi chetu ni imara na chama chetu kinaheshimika kitaifa na kimataifa vijana njooni ccm nyumbani ni nyumbani "- Shaka.

" Huu ni wakati sahihi kwa vijana wasomi weye  elimu za juu, kati  na wenye elimu za  kawaida kuuuga mkono sera za chama tawala ili kujenga shime mpya  ya kukuza  utaifa na uzalendo wa kweli" - Shaka

"Sisi vijana tunatakiwa kusimama bega kwa bega na Rais Magufuli kumsaidia yale yote anayoyakusudia kuyatekeleza kisera tumpe nguvu na jeuri ya kutenda huku tukipaza sauti kupinga rushwa, ubadhirifu wa mali za umma, maonevu, kulinda  rasilimali zetu hatimaye   huduma za jamii ziimarike "- Shaka

" Itoshe kwa vijana wote kujipima na kujitambua huko waliko kwenye upinzani iwapo kuna matarajio na matumaini yenye uzito na kama wamebaini ni kufuja wakati warudi kwenye chama cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere " - Shaka

"Njooni huku kwani  CCM ndicho chama tulichoachiwa na muasisi  wa Taifa letu Mwalimu Nyerere na wenzake kina Mzee Karume, Rashidi Kawawa, Aboud Jumbe,  Thabit Kombo, Rajab Diwani, Daud Mwakawago, Lucy Lamerck na Titi Mohamed na bado ni  imara  na kiko katika mikono salama ya nahodha mahiri, shupavu na mweledi Dk John Pombe Joseph Magufuli "-  Shaka

*Jana aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro 2012 na kujiunga CHADEMA 2015 Fedrick Elifuraha  Mushi alirudi Kujiunga na CCM ambae alipokelewa na Katibu wa    CCM  mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabiya.*
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top