Mstahiki meya wa manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitaa amewaeleza Wananchi wa kata za Mbezi Jogoo, Salasala na Kinzudi kuwa ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Salasala Kwenda Kinzudi kuanza maramoja na kwamba atahakikisha unakamilika ndani ya muda ya mchache.
Barabara hiyo yenye urefu wa Kilomita 1 imekuwa kero kubwa kwa zaidi miongo miwili kwa wakazi wa maeneo hayo.
Aidha Mheshimiwa sitta amesema kuwa barabara nyingi katika manispaa hiyo zimejengwa chini ya kiwango na kwamba wamewataka wakandarasi wa miradi hiyo kurudia ujenzi huo kwa gharama zao.
Hata hivyo kutokupimwa kwa maeneo katika kata ya Mbezi Jogoo, Salasala na Kinzudi, suala la maji, Kiwanja cha Michezo, uwekaji wazi wa taarifa kwa Wananchi na mifugo Vimetajwa kama changamoto kubwa katika maeneo hayo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Viongozi na Wananchi kutoka katika vyama vyote vya Siasa.
Post a Comment