Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Morogoro mjini Abdulaziz Abood pamoja na Mkuu wa wilaya ya Morogoro wakifanya ukaguzi wa barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa barabara za lami Manispaa ya Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Morogoro wakikagua maandalizi ya ujenzi wa barabara za lami zinazoendelea kujengwa.
Meneja wa Tarura Manispaa ya Morogoro akitoa maelekezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipotembelea kukagua maandalizi ya ujenzi wa barabara za lami.
…………….
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amemtaka meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini(TARURA) Manispaa ya Morogoro kuhakikisha barabara za lami zinazojengwa ndani ya manispaa hiyo zinakuwa katika ubora unaotakiwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu.
Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa akikagua miradi ya ujenzi wa barabara hizo huku akibaini kuharibika kwa baadhi ya barabara za lami zilizojengwa miaka michache iliyopita.
Amesema kuwa ujenzi wa barabara za lami umekuwa ukitumia gharama kubwa hivyo ni vyema Meneja huyo akahakikisha anasimamia ili ujenzi wake uwe kwenye viwango vinavyotakiwa.
“Haiwezekani tunatumia fedha nyingi lakini barabara zinaharibika ndani ya muda mfupi wakati wahandisi mnaosimamia mpo.Sitamvumilia mhandisi yeyote kwa miradi inayojengwa endapo haitakidhi viwango,”amesema Jafo.
Jafo amewaonya mameneja ya TARURA wa wilaya ambao watashindwa kusimamia kazi zao ipasavyo katika halmashauri zao wanazozisimamia kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua.
Post a Comment