Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amewataka wagombea wote wa udiwani katika kata tano Arumeru Mashariki wajitoe katika uchaguzi huo.
Mbowe ametoa rai hiyo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha huku akisema kuwa uchaguzi huo umegubikwa na vurugu.
Sambamba na hayo Freeman Mbowe amewataka mawakala wao wa uchaguzi katika vitup vya kupigia kura waondoke vituoni.
Leo wananchi wa Tanzania Bara wanapiga kura kuchagua madiwani katika kata 43 hapa nchini, lakini mpaka sasa kumekuwa na taarifa mbali mbali za uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo kukamatwa ka baadhi ya wagombea na mawakala.
Loading...
Post a Comment