MHE. BASHE AFANYA MKUTANO WA HADHARA NA WANANCHI - NZEGA MJINI
Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Mohammed Bashe amekua na mkutano wa wazi na wananchi uliojikita katika kuelezea mafanikio na changamoto za miaka miwili ya kipindi cha ubunge wake.
Aidha Malengo makubwa ya mkutano huo yalikuwa ni:
1. Kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa uwazi ili kuongeza nafasi ya ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika mijadala ya maendeleo.
2. Kueleza juhudi za kuleta maendeleo zilizokwishafanywa na Ofisi ya Mbunge katika kipindi cha miaka miwili (2)
3. Kutambulisha miradi mikubwa ya Elimu, Afya na Maji inayoendelea ndani ya Jimbo la Nzega Mjini;
Elimu
- Ujenzi wa Shule ya kwanza ya wanawake
- Utoaji wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wanaofaulu Jimboni kupitia Bashe Scholarship Awards
- Ugawaji wa Vifaa vya shule na madaftari 37,000
- Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya Kidato cha Tano na Sita
- Ujenzi wa zaidi ya vyumba vya madarasa 32 ya Shule za Msingi kwenye kata 10 jimboni
Afya
- Ujenzi wa Nyumba za waganga
- Ujenzi wa Zahanati kwenye kila Kata
- Ugawaji wa Vitambulisho vya Matibabu kwa wazee
- Upanuzi wa kituo cha Afya cha Zogolo kuwa na hadhi ya Hospitali
4. Kuelezea miradi ya uwezeshaji kwa akina mama na vikundi vya wajasiriamali ambayo imefanywa na Ofisi ya Mbunge ikiwemo;
- Utoaji wa mikopo kwa vijana
- Utoaji wa mikopo kwa wanawake
- Utoaji wa pikipiki kwa vijana
5. Kuelezea mradi mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria ambao tayari umeshaanza utekelezaji wake hivyo kuwahamasisha wananchi kulinda mali na kuwa tayari kupisha maeneo ambayo mradi utapita ili kuweza kutatua kanisa shida ya Maji Nzega.
6. Upatikanaji wa fedha za Maendeleo zaidi ya Bilioni Moja na Milioni Mia Tank nje ya Bajeti.
(a) 259,000,000 - Ujenzi Shule ya Bweni ya Kwanza Nzega ya Kidato cha Tano na Sita
(b) 384,000,000 - Ujenzi wa Shule ya Kwanza ya wasichana Nzega Kidato cha Kwanza hadi Sita
(c) 400,000,000 - Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji. Fedha hizi amezitoa Mhe. Dr. John Pombe Magufuli baada ya kumuomba alipotembelea kwa nyakati tofauti Nzega na Tabora.
(d) 500,000,000 - Ujenzi na Upanuzi wa Kituo cha Afya cha Zogolo kuwa na hadhi ya hospitali.
7. Kuelezea mafanikio na maendeleo makubwa ya ukuaji wa sekta ya elimu ndani ya Jimbo la Nzega Mjini kwa kipindi cha miaka miwili tangu amekua Mbunge kama ifuatavyo;
Ufaulu Elimu ya Msingi Nzega
2014 - 48%
2015 - 54%
2016 - 74%
2017 - 90.66%
Ufaulu Elimu Sekondari IV
2014 - 59%
2015 - 72%
2016 - 77%
2017 - 82%
Ufaulu Elimu Sekondari II
2015 - 79%
2016 - 81%
2017 - 87%
Mwisho; Mhe Hussein Bashe ameunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kusimamia rasilimali; kufunga mianya ya rushwa na kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
Kwa upande mwingine Mhe. Bashe amemshukuru Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa Namna ambavyo amekua bega kwa bega katika kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Nzega Mjini kutatua changamoto mbalimbali.
Mheshimiwa Bashe amesema ya kuwa ...."Mwaka 2015 katika viwanja hivi vya parking nikiwa na Mgombea urais wakati huo Mhe. John Pombe Magufuli nilimuahidi kuwa Mimi sitakua mbunge wa ndio Mzee ila nitamsaidia sana katika kuishauri serikali, kuitetea na pia kuikosoa pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa serikali na Chama cha Mapinduzi."
Post a Comment