Loading...
UVCCM wazungumzia kilichojili kikao cha NEC - CCM
TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI ILIYOTOLEWA NA KAIMU KATIBU MKUU WA UMOJA WA VIJANA WA CCM SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC) KWA VYOMBO VYA HABARI, JUMATANO 22 NOVEMBA 2017. UPANGA, DAR ES SAALAM
Ndugu Waandishi wa Habari
Umoja wa Vijana wa CCM tunakipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kuonyesha umadhubuti na uimara wake kidemokrasia na kisiasa chini ya kiongozi shupavu na mweledi Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Joseph Pombe Magufuli.
Ni wazi kuwa Chama chetu kipevuka na kukomaa kisiasa juu ya uendeshaji wake katika dhana na misingi ya demokrasia, uwazi katika ushiriki wa wanachama kukitumikia na kufanya maamuzi muhimu yanayohusu mustakabali wa chama chao.
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) tunasifu umadhubuti na ujasiri wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Joseph Pombe Magufuli kwa kukiongoza chama Cha Mapinduzi, kufuata na kujali uhuru wa mawazo, kuheshimu mipaka ya demokrasia na kuthamini heshima ya kila mwanachama katika kuenzi haki na uthubutu wa kila mmoja.
Msingi wa kuwepo fursa ya Uhuru mkubwa wa ukusanyaji mawazo, mapokeo ya fikra na uchukuaji maoni na kusikiliza ushauri wa kila mwanachama kwa upana wake ni salama na ishara pekee ya ukomavu na ni dalili ya upevu halisia wa ustawi wa demokrasia shirikishi.
Uvccm tunaamini kuwa Chama Cha Mapinduzi kwa asili yake tokea enzi za TANU na ASP ni chenye kufuata na kuheshimu misingi ya haki, usawa huku kikipinga ubaguzi wa rangi, kukataa ukabila, udini na ukanda huku kikiheshumu na kufuata miiko ya demokrasia na kuidumisha.
Tunachukua nafasi kuwapongeza wajumbe wote wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kwa kuithibitishia dunia CCM ni ngome na mlezi wa demokrasia kwani tumefarijika kukiona chama chetu kikibaki na heshima yake ya asili.
Chama Cha Mapinduzi chini ya utawala na utendaji wa Serikali ya inazoziongoza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kimekuwa katika jitihada kubwa ya kupigania maslahi ya umma, kutunza rasiliamli za Taifa katika dhamira ya kupambana na uhujumu uchumi, ufisadi na kusimamisha dhana ya uwajibikaji, utumishi unaojali haki za watu masikini na wanyonge kitaendelea kuvuna idadi kubwa ya wanachama.
Umoja wa vijana wa CCM tunafurahia kuona utamaduni uliopo ndani ya CCM hauwezi kupatikana mahali popote duniani katika aina ya uendeshaji wa masuala ya siasa na utawala hivyo ni jukumu la kila mtanzania sasa kukiunga mkono chama tawala CCM .
Kimsingi na kiuhalisia UVCCM tunajua na kujivunia tuna chama chenye viongozi wanaongozwa na busara, hekima na ukomavu wa kisiasa katika msuala ya utawala, siasa na uongozi. UVCCM tunaahidi na kuuhakikishia umma kuwa tafuata nyayo hizo katika na kuhakikisha chama chetu kinashinda na kuendelea kuongoza Taifa kwa njia ya kidemokrasia .
Umoja wa Vijana wa CCM tutaendelea kujivunia ubora na umakini wa chama chetu mahali popote. Tunasifu ujasiri na uwezo mkubwa alionao Mwenyekiti wetu Dk John Joseph Pombe Magufuli tunaamini tupo katika mikono salama na katu hatutayumbishwa na vyama vya upinzani.
Ndugu waandishi wa Habari.
Umoja wa Vijana wa CCM tunapongeza na kuunga mkono maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM Dk Magufuli ya kujipa muda wa kutafakari na hatimae kumrudisha uanachama wake aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba uamuzi huo umeidhihirishia dunia kuwa ndani ya CCM kuna ukomavu mkubwa wa maendeleo ya demokrasia sambamba na kuheshimu katiba, kanuni na miongozo iliyojiwekea.
Kuhusu uamuzi na hatua ya baadhi ya wanachama kurudi na wengine kujiunga upya na CCM toka vyama vya CHADEMA na ACT Wazalendo tunaamini wananchi hao wamerudi mahali salama tena kwenye uhakika mkubwa kuliko huko walikokuwa.
Ndugu Waandishi wa habari.
Napenda kuzungumzia maendeleo ya Uchaguzi wa UVCCM unaendelea hasa wakati huu muhimu na kihistoria kuelekea ukingoni kuhitimisha chaguzi za jumuiya yetu zilizoanza kwenye matawi hadi wilaya mapema April 2017, sasa tukielekea kukamilisha mikutano mikuu ili kuwapata viongozi wa mikoa na kitaifa.
Nichukue nafasi hii kuwapongeza sana watendaji wetu wa Jumuiya ngazi mbali mbali kwa kusimamia vyema chaguzi kwenye maeneo yao na kufanikisha vizuri licha ya kujitokeza kasoro na mapungufu madogo ya hapa na pale.
Jumuiya yetu ya vijana wa CCM (UVCCM) mwakan inatimiza miaka 40 tokea ilipoanzishwa mwaka 1978 kufuatia tukio la kihistoria la kuungana kwa vyama vya ukombozi vya TANU na ASP.
Jumuiya yetu licha ya kupevuka na kukomaa imepata mafanikio makubwa ya Nyanja za kisiasa, kiutawala na kiuongozi kwa kuwatayarisha na kuandaa viongozi ambao wengi wao ndiyo waliopewa dhamana za uongozi wa nchi kwenye nyanja mbalimbali za kiserikali na kisiasa.
Tunakutana nanyi leo tukiwa kwenye hatua za mwisho mwisho kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu wa (9) Tisa wa Umoja wa Vijana wa CCM utakaotoa mwelekeo halisi wa kuwapata viongozi watakaoingoza Jumuiya kwa kipindi cha miaka mitano 2017-2022
Tokea wakati tulipoanza michakato ya chaguzi zetu ngazi za matawi hadi Taifa tumekuwa tukiwaeleza, kuwaonya na kuwakataza mara kwa mara tena bila kuchoka na kuwataka wanajumuiya wanaogombea nafasi mbali mbali za uongozi kufuata na kuheshimu kanuni za uchaguzi bila kuzikiuka na kutovunja miiko.
Nachukaa tena nafasi kuwaasa na kuwataka wale wote walioteuliwa na vikao mbali mbali waendelee kuheshimu na kufuata taratibu na kanuni za uchaguzi tunawashauri kuendelea kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa na chama na jumuiya. Ikumbukwe kuwa mgombea kuteuliwa si kigezo cha kutotenguliwa ikiwa atathibitika amevunja na kukiuka kanuni, katiba na taratibu.
Bado wagombea wote walioteuliwa na chama wataendelea kufuatiliwa kwa karibu mno na kwa umakini wa hali ya juu Vyombo vyetu vya chama na serikali havitajiweka mbali na mienendo yao
Jumla ya Vijana 7,590 walijitokeza kuchukua fomu za kuomba nafasi mbali mbali za uongozi ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM kati nafasi 206 kitendo kilichoonesha na kudhihirisha namna gani vijana wanakiunga mkono Chama Cha Mapinduzi na jumuiya Umoja wa Vijana wa CCM.
Baada ya kukamilika kwa utaratibu wa vikao vyote vya uchujaji Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM katika kikao chake cha tarehe 17 Oktoba 2017.
Naomba kutaja vijana walioteuliwa na kikao cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa ambao ni:-
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU
Post a Comment