Dodoma. Jumla ya wakazi 1,172 wanaoishi katika vijiji vitano vilivyopo
jirani na Ikulu Chamwino mkoani hapa wamenufaika na mafunzo ya
kuwaongezea ujuzi ili washiriki vyema katika upanuzi wa makazi ya
Rais.
Neema hiyo imefuatia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli
alilolitoa Julai mwaka jana mjini hapa la Serikali kuhamia mkoani hapa
kabla ya awamu ya kwanza ya uongozi wake kukamilika.
Tayari Waziri Mkuu, mawaziri, manaibu, makatibu wakuu, manaibu
makatibu wakuu na baadhi ya watumishi wameshahamia mjini hapa ikiwa ni
utekelezaji wa agizo hilo.
Akizungumza katika mahafali ya tisa ya Chuo cha Veta mkoani hapa, Mkuu
wa chuo hicho Ramadhan Mataka amesema kuwa mafunzo hayo yaliendeshwa
chini ya mfumo wa Competent Based Education and Training (CBET).
“Tumeshirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao
tumeshirikiana nao katika kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa baadhi ya
washiriki 1,172 kutoka katika vijiji vitano kwa lengo la kuwaongezea
ujuzi ili washiriki vyema katika upanuzi wa Ikulu ya Chamwino,” amesema
Mataka.
Mataka amesema pia chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Kazi Ajira,
Vijana na Watu wenye Ulemavu wamewatambua wanagenzi 260 ambao kati ya
hao 241 wamefaulu baada ya kupimwa mkoani Dodoma.
Akizungumzia kuhusu programu hiyo ya wanagenzi, Naibu Waziri katika
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana Antony Mavunde amesema chini
ya programu hiyo wanawachukua wakufunzi wa Veta na kwenda nao mtaani
kwa ajili ya kubaini mapungufu waliyonayo vijana na kuyaziba.
“Baadaye vijana hao tunawapa vyeti vya Veta bila kusoma Veta. Hawa ni
vijana 3,900 ambao wako mitaani,”amesema
on Thursday, November 23, 2017
Post a Comment