Loading...
WALEMAVU WALIOKIMBILIA KWA RC MAKONDA SASA WAANZA KUPATA NEEMA
Hospitali ya *CCBRT* imeguswa na Kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mheshimiwa PAUL MAKONDA* ya kutafuta Miguu Bandia kwa *watu wenye uhitaji* kwa kuwapatia matibabu *Wagonjwa 35* waliokatwa Miguu kutokana na *Ugonjwa wa kisukari.*
Miguu hiyo ya kisasa ina thamani ya zaidi ya *Shilling Million 157* ambapo Kati ya *Wagonjwa 35* waliokuwa wakitembelea *Magongo* kwa muda mrefu baada ya kukatwa miguu, *21 wameshawekewa Miguu Bandia na sasa wanaendelea na Shuguli zao* baada ya kuwa wazima.
*RC MAKONDA* amesema lengo la kampeni hiyo ni *kusaidia wanaotumia Magongo kupata Miguu ya Bandia ya kisasa ili waweze kuendelea na shughuli zao ujenzi wa Taifa* na kuhudumia Familia.
Ameishukuru *Hospital ya CCBRT* kwa kuunga mkono kampeni hiyo pamoja *E FM RADIO* na *TV E* walioojitolea kuhamasisha jamii kuchangia Miguu Bandia.
Katika hatua nyingine *RC MAKONDA* amepatiwa kiasi cha *Shillingi Million 10,000,000* kutoka kampuni ya Ujenzi ya *SPECTUM DESIGN* ambapo Mkurugenzi wake *Arch.JIMMY MKENDA* amesema lengo la kutoa mchango huo ni baada ya *kuguswa na kampeni hiyo* inayolenga kuwasaidia *waliokata tamaa baada ya kupoteza miguu*.
Aidha *RC MAKONDA* amesema kuwa atazungumza na *Taasisi zinazotoa Bima ya Afya* ili waongeze kipengele cha *Matibabu na kutoa Miguu bandia* kwa watu waliopoteza Miguu kwa *Ajali au Ugonjwa.*
Amehamasisha jamii kuchangia kampeni hiyo kupitia *CRDB* account namba *0150299713500* au kufika ofisi za Mkuu wa Mkoa au E FM Radio kisha kuwasilisha mchango wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa walemavu Hospital ya CCBRT *BRENDA MSANGI* amewaasa *Wananchi kuchangia kampeni hiyo* huku akieleza kuwa *wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa.*
Post a Comment