Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Mh. Zitto Kabwe, leo ameripoti kituo cha Polisi Chang’ombe kama alivyotakiwa baada kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana Oktoba 31, 2017. Baada ya kuripoti Polisi wamemueleza kuwa anapaswa kuripoti tena kituoni hapo Ijumaa ijayo, Novemba 17 mwaka huu.
Katibu wa Itikadi, Mwasiliano ya Umma na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu ameeleza kuwa Kadhia hii inahusisha baadhi ya maneno katika hotuba yake ya Oktoba 29, 2017 alipokuwa kwenye mkutano wa kuzindua kampeni za udiwani katika Kata ya Kijichi, Wilayani Temeke. Maneno hayo ni yafuatayo:
1.Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu mpaka siku hiyo.
2.Kwamba wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.
Mh. Ndugu Zitto aliongozana na timu ya mawakili wa chama pamoja na mke wake kituoni Chang’ombe.
Post a Comment