Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi (PSPTB) uliofanyika jijini Arusha leo(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt Philip Mpango akizungumza katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho akizungumza katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh.Anna Mghwira akiwa katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo akiteta jambo na Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan katika kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Wadau wa mkutano huo wakifatilia kwa ukaribu
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa kongamano la nane la wataalamu wa ununuzi na ugavi uliofanyika jijini Arusha leo.
Na Pamela Mollel,Arusha
Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya fedha na mipango kuhakikisha wanakamilisha mapema sera yaTaifa ya Ununuzi wa Umma kwa kufanya marekebisho ya sheria ,kanunina taratibu zingine zikakazo ongoza shughuli za ununuzi wa umma hapa nchini
Akizungumza leo jijini Arusha katika kongamano la nane la wanataaluma ya ununuzi na ugavi(PSPTB)iliyowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wadau kutoka nchi jirani ya Kenya
Bi.Samia alisema kuwa kwa kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma utasaidia kuongeza kiwango cha uwajibikaji wa wadau wote wanaohusika katika shughuli za umma
Aidha aliongeza kuwa ripoti mbalimbali za ukaguzi zinaonyesha kuwa Serikali imeendelea kupata hasara katika eneo la ununuzi wa umma kutokana na wataaluma wachache kutokuwa tayari kutimiza wajibu wao au shughuli hizo kufanywa na watu wasio na taaluma hiyo
“Napenda kuwaasa ambao bado wanaendeleza vitendo viovu kama rushwa ,upendeleo,wizi,uzembe waache mara moja na watambue kuwa sheria zipo na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao”alisema Bi.Samia
Pia alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano haitamvumilia mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na maadili ya taaluma yake
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na mipango(Mb)Dkt Philip Mpango alibainisha mapungufu yaliyoonekana katika taasisi zilizokaguliwa ikiwemo kupungua kwa kiwango cha uzingatiaji wa sheria ya ununuzi wa umma katika Halmashauri kutoka wastani wa asilimia 71 mwaka 2015-16 hadi asilimia 69
Pia Mh.Mpangoalisema kuwa miradi 7iliyokaguliwa yenyethamani ya shilingi bilioni 2.37 imebainika kufanywa chini ya viwangovisivyoridhisha
Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa maadili ya ukaguzi umebaini kuwepo kwa viashiria vingi vya rushwa katika usimamiziwa miradi 33 katika taasisi 17 za Umma zilizokaguliwa hivi karibuni
Naye Mwenyekiti wa bodi ya PSPTB Dkt.Hellen Bandiho alisema kuwa changamoto inayoikabili bodi hiyo kwa sasa ni pamoja na waajiri kuajiri watumishi wa ununuzi na ugavi ambao hawajasajiliwa na bodi.
Post a Comment