SIKU mbili baada ya kujiuzulu ubunge, kung’atuka CUF na leo kujiunga CCM, Maulid Mtulia amesema yeye ni mwanajeshi na yupo tayari kwa kazi yoyote atakayopewa na chama hicho, ikishindikana atakwenda kulima kijijini kwao wilayani Rufiji.
Maulid Mtulia akionyesha kadi yake ya CCM mara baada ya kujiunga na chama hicho hii leo jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika mahojiano maalum na matukio360 hii leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kujiunga CCM amesema hawezi kukubali au kukataa kama atagombea tena ubunge katika jimbo hilo.
"Elewa mimi ni mwanajeshi nipo tayari kufanya kazi yoyote ndani ya CCM. Kama nitagombea ubunge ama la, muda wa hilo bado. Kutangaza nia kuna muda wake,’’ amesema Mtulia
Amesema hata kama CCM haitompa kazi ya kufanya atakwenda kijijini kwao katika wilaya ya Rufiji kulima.
“Hata kama CCM haitonipa kazi ya kufanya nitakwenda kwetu Rufiji kulima,’’ amesema
Awali baada ya kukabidhiwa kadi Mtulia amesema:
"Nimejivua nyadhifa zangu zote ya Ubunge wa Kinondoni na vyeo vyote nilivyokuwa navyo CUF na kuamua kujiunga na CCM kutokana na kuridhishwa na CCM ya sasa na utendaji wa Rais Dk. Magufuli"
"Mimi ni mgeni na salamu ninayoijua ya CCM ni CCM Oyeee"
"Nimejiunga na CCM ili kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na Rais Dk. Magufuli"
"Nimetoka kwenye chama chenye migogoro mingi, nimekuja kwenye chama chenye amani, haki na Demokrasia ya kweli"
"Ningekuwa Mbunge kupitia CCM ningefanya mengi makubwa zaidi"
"Sijaja CCM kutafuta cheo bali nimetumia haki yangu ya kidemokrasia ya kujiunga na chama chochote kile ninachokitaka"
"Kila jambo nililokuwa namwomba Rais tena hadharani (mfano wakati wa ufunguzi wa maghorofa) ameyatekeleza kwa kiwango kikubwa" -
"Nawashangaa Viongozi wa Upinzani wanaopinga na kususa mambo ya Serikali na shughuli za Bunge, hizo shida za Wananchi Nani atawatatulia endapo wanawasusia wenye mamlaka?"
"Nipo tayari kuwa hata Balozi wa nyumba kumi na ikishindikana nitaenda kuvua samaki nyumbani Rufiji" - Mtulia
"Nawahaidi wana CCM watafurahia uwepo wangu na watanufaika nami ndani ya CCM"
"Nawaambia wana Kinondoni wasikosee, wachague Mbunge anayetokana na CCM. Wachague CCM siku zote" -
Post a Comment