Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewapa onyo la mwisho Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuwataka wawe wasimamizi wazuri wa fedha za nchi na kusema kama hawatajirekebisha basi wasijekumlaumu siku za usoni.
Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizindua tawi moja la Benki mjini Dodoma na kuzitaka benki zote pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuangalia suala la matumizi ya fedha za kigeni ndani ya nchi kwani jambo hilo linazidi kuuwa uchumi wa nchi.
"Haiwezekani nchi ikawa na 'curency' mbili, tatu au zaidi zinazotumika zinaharibu uchumi, haiwezekani mtu ukiwa na dollar unakwenda kununua bidhaa dukani, ukiwa na pounds unakwenda kununua chochote nchini huu si utaratibu wa uchumi. Na hili nikuombe Waziri, BoT na mabenki yote mlisimamie hili kikamilifu, na baya zaidi haya yamekuwa yakifanywa na BoT. Gavana upo hapa mnapotangaza tenda zenu hata za wafagiaji mnawalipa kwa Dollar .
"Sasa haiwezekani nyinyi BoT ambao mnasimamia fedha nyinyi hao hao mnakuwa wabaya wa kudhibiti fedha za nchi hili lazima muende nalo na mbadilishe haraka.
"Msije kuwa chanzo cha kuharibu uchumi wa nchi yetu. Najua mnanielewa nililizungumza jambo hili mara ya kwanza nimelirudia leo mara ya mwisho litakalotokea msije kunilaumu" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli amehitaji kuwe na uangalizi mzuri kwenye 'Bureau de Change' na kuwa na utaratibu ambao unaeleweka.
Post a Comment