Serikali inatarajia kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha miundombinu ya umeme na upatikanaji wa uhakika kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya kikazi Wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua na kujionea miundombinu ya umeme wa Rea awamu ya tatu ,Waziri wa Nishati ,Dr Medadi Kalemani ,alisema kuwa hali ya umeme inaendelea kuimarika siku hadi siku na kuna maeneo mengi yameanza kupata umeme wa kutosha.
“Hapo Nyuma mwezi Novemba tulikuwa tunajitahidi kukarabati mahali ambapo kulikuwa na ubovu wa mitambo lakini kwa sasa hali inaendelea vizuri maeneo mengi ya nchi yetu yanapata umeme kwa wingi na tunaanza kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha miundo mbinu ya umeme na upatikanaji wa umeme hapa nchini”Alisema Kalemani.
Aidha Dr,Kaleman amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye maeneo yao pindi kunapotoakea tatizo na kwamba wateja ambao wamelipia umeme kwa mwaka 2017 ni vyema Tanesco wakahakikisha wanawaunganishia umeme haraka iwezekanavyo kwani mwaka 2018 haitakiwi kuwepo kwa mteja ambaye ajaunganishiwa huduma hiyo.
Post a Comment