YALIYOSEMWA NA KAIMU KATIBU UVCCM SHAKA H. SHAKA WAKATI AKITAJA WAJUMBE WA KAMATI YA KUCHUNGUZA NA KUFUATILIA MALI NA RASILIMALI ZA UVCCM
"Tunawashukuru Waandishi wa Habari kuwa bega kwa bega na UVCCM nyakati zote na hata wakati wa Mkutano Mkuu mlihakikisha taarifa zinafika kwa Wanachama, wapenzi, Watanzania na Dunia kwa ujumla." - Shaka
"Moja ya ajenda kuu aliyoanza nayo ni ya Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri James ni kuhakikisha anamuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na kuendana na matakwa ya UVCCM ni kusimamia rasilimali, vitega uchumi pamoja na vianzio vyote vya mapato vya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi" - Shaka
"Mwenyekiti Kheri amedhamiria kusimamia maslahi mapana ya CCM na ya UVCCM kwa kufanya mabadiliko makubwa ya kimfumo, kiutawala na kiundeshaji" - Shaka
"Sote tunafahamu UVCCM ndio kimbilio, ndio tumaini LA Vijana wote pasipo kujali itikadi wala hadhi zao toka UVCCM inaanzishwa mwaka 1978" - Shaka
"UVCCM imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia rasilimali za UVCCM nchini kote. Kamati hii ni maarufu kwa jina la "Kamati ya Makinikia UVCCM" - Shaka
"Wajumbe wa Kamati hii wanaoenda kuchunguza na kufuatilia rasilimali na Mali za UVCCM ni:-
1. Ndugu Mariam Khatibu Chaurembo - Mwenyekiti wa Kamati hii
2. Ndugu Peter Kasera - Mjumbe
3. Ndugu Zailote Saitoti - Mjumbe
4. Ndugu Rose Manumba - Mjumbe
5. Ndugu Sophia Kizigo - Mjumbe
6. Ndugu Elliah Ngowi - Mjumbe
" - Shaka
"Wajumbe wengine wawili (2) wataungana na wengine baadae Mara baada ya kutangazwa rasmi ili kukamilisha idadi kamili ya Wajumbe 8" - Shaka
"Kamati hii inaanza rasmi kazi Mara moja ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli. Kamati hii watapewa mwongozo ndani ya kipindi kifupi sana na watajulishwa namna ya kufanya kazi na hadibu za rejea zipo tayari." - Shaka
"Pindi watakapo kamilisha Watanzania na kila mtu watapata taarifa ya ripoti ya kamati hiyo" - Shaka
Shaka Hamdu Shaka ni Kaimu Katibu Mkuu UVCCM aliyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisi ndogo Makao Makuu ya UVCCM Upanga Ijumaa Disemba 22, 2017
on Friday, December 22, 2017
Post a Comment