Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mpango: "Uchumi umekuwa sana"



YALIYOJIRI WAKATI WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHE. DKT. PHILIP MPANGO AKITOA TAARIFA YA HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI 2017/18, LEO IJUMAA DISEMBA 29,2017.
_______________________________
01. "Leo tunatoa taarifa ya mwenendo wa uchumi wa Taifa kuanzia mwezi Januari hadi June, 2017" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

02. "Pia tutafafanua utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha pamoja na changamoto na matarajio ya Serikali" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

03. "Pia taarifa hii inatoa ufafanuzi katika baadhi ya maeneo yanayopotoshwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

04. "Kiashiria cha ukuaji wa uchumi ni ukuaji wa Pato la Taifa" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

05. "Pato la Taifa la nusu ya kwanza ya mwaka umekua kufikia 6.8%" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

04. "Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ya asilimia 2.7 kwa mwaka hivyo kusababisha Pato la Taifa kugawanywa kwa watu wengi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

05. "Ikilinganishwa na nchi zingine za Afrika Mashariki, Tanzania bado ni kinara kwa ukuaji wa uchumi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

06. "Katika nchi 7 bora za Afrika kwa kasi ya ukuaji wa uchumi, Tanzania ni moja wapo" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

07. "Kwa mwaka mzima wa 2017 tunakadiria uchumi kukua kwa 7%" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

08. "Mfumuko wa bei umeendelea kubaki katika kiwango kizuri cha tarakimu moja. Wastani wa mfumuko huo kutoka Januari hadi Novemba ni 5.4%" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

09. "Kwa mwezi Novemba mwaka huu, mfumuko wa bei ulipungua zaidi kufikia 4.4%" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

10. "Thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani kwa mwaka 2017 imeendelea kuimarika" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

11. "Akiba ya fedha za kigeni imefikia Dola za Kimarekani Milioni 5911.2 kiasi kinacholiwezesha Taifa kununua vitu kwa miezi 5.4" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

12. "Kiasi hiki kipo juu ya lengo la nchi wanachama wa Afrika Mashariki ambacho kiasi kinachotakiwa kuwepo ni cha kuliwezesha Taifa kununua vitu kwa Miezi 4.5" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

13. "Napenda kuwapongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa Sera za Fedha unaohakikisha thamani ya Shilingi haimomonyoki" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

14. "Kuanzia Disemba 12 mwaka huu Benki Kuu ya Tanzania imeshusha riba inayoitoza Serikali katika mikopo kutoka 6.5% hadi 3% ili kuchochea utoaji wa Mikopo katika uchumi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

15. "Napenda kuwahakikishia Wananchi kuwa sekta za kibenki zimeendelea kuwa imara na salama" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

16. "Serikali inazitaka benki za biashara kuchukua hatua za makusudi kushusha riba za mikopo na kuzingatia kanuni za ukopeshaji" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

17. "Serikali inashauri benki za biashara kupunguza masharti ya mikopo kwa vikundi vilivyosajiliwa" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

18. "Baada ya kubana mianya ya rushwa, Serikali inakusanya wastani wa trilioni 1.2 kila mwezi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

20. "Tunawashukuru wafanyabiashara wote wanaolipa kodi kwa uhakika, tunatoa rai kwa Watanzania kujijengea utamaduni wa kulipa kodi ipasavyo" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

21. "Katika matumizi ya fedha,tumetoa Shilingi bilioni 135.7 kwa ajili ya usambazaji wa Umeme Vijijini (REA)" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

22. "Tumetoa fedha kwa baadhi ya miradi mingine ikiwemo ya Elimu bila malipo Bilioni 78.5, mfuko wa reli Bilioni 69.9, mfuko wa maji Bilioni 64.6, pamoja na ununuzi wa madawa" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

23. "Tathmini ya uhimilivu wa deni ililofanyika Novemba, 2017 inaonesha uwiano wa Deni kwa Pato la Taifa ni 32.5% ikilinganishwa na ukomo wa 56% ambao unamaanisha deni la Taifa lipo chini ya ukomo wa hatari na ni himilivu -  Dkt. Mpango.

24. "Mapato ya kodi yameongezeka kufikia Bilioni 4,067.4 ikilinganishwa na Bilioni 4,033.1 zilizokusanywa katika kipindi cha mwaka 2016/17" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

25. "Kati ya makusanyo hayo,mapato ya kodi ni Bilioni 3,564, mapato yasiyo ya kodi Bilioni 378.7 na mapato ya Halmashauri Bilioni 124.7" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

26. "Mchango wa misaada na mikopo ya masharti nafuu katika Bajeti ya Serikali umepungua, kwa mwaka 2017/18 jumla ya Bilioni 3,971.1 iliahidiwa na Washirika wa Maendeleo ambayo ni sawa na 12.5% ya Bajeti nzima" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

27. "Serikali inaamini kuwa maendeleo endelevu yatapatikana kwa haraka kama kuna mashauriano kati ya Serikali na sekta binafsi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

28. "Tayari Serikali imeandaa mpango kazi ambao utekelezaji wake utawezesha kupunguza au kuondoa kero zinazoikabili sekta binafsi" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

29. "Ili kulinda shilingi ya Tanzania, Serikali imetoa maagizo yatakayoanza kutekelezwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

30. "Bei zote nchini kutangazwa kwa shilingi ya Tanzania, viwango vya kubadilishana fedha visizidi vile vya soko, wakazi wa Tanzania wasilazimishwe kulipia huduma au bidhaa nchini kwa fedha za kigeni" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

31. "Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na kulipwa kwa fedha za kigeni" - Mhe. Dkt. Philip Mpango.

IMEANDALIWA NA:-
IDARA YA HABARI - MAELEZO.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top