Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Zitto afanya mazungumzo na Viongozi wa Ukawa



Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa juu wa vyama vinavyoundwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Viongozi waliofanya mazungumzo na mbunge huyo wa Kigoma Mjini ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pamoja na Mwenyekiti wa Chaumma, Hashim Rungwe ambaye hivi katibuni alialikwa Ukawa kujadili kasoro za uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika hivi karibuni. Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema, NLD, CUF na NCCR-Mageuzi na vyote vimetangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika Januari 13, 2018.

Katika taarifa yake, Zitto alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuagizwa na uongozi wa Taifa wa ACT-Wazalendo uliomtaka kuwafikia wadau wote wa demokrasia na kuweka mikakati ya pamoja.

“Uongozi wa Taifa wa ACT-Wazalendo umeanzisha mazungumzo na vyama vyote vya upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vinavyofanywa na chama tawala vya kuvuruga chaguzi huru na za haki,” alisema Zitto.

Mwanasiasa huyo alisema wakati Katibu Mkuu wa chama hicho, Dorothy Semu akiendelea na utaratibu rasmi wa kutekeleza jambo hilo, yeye alipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo na viongozi wa juu wa Ukawa.

“Jana (juzi), nimezungumza na Mbatia aliye hospitalini KCMC–Moshi baada ya ajali, namuomba Mola ampe afya njema. Pia nilikutana na Mbowe na nina furaha mazungumzo yetu yameanza vizuri,” alisema Zitto ambaye aliwahi kuwa naibu katibu mkuu wa Chadema kabla ya kuondoka na kuanzisha ACT-Wazalendo.

Kiongozi huyo pia alikutana na Rungwe na kufanya naye mazungumzo.

“Mazungumzo yetu yatazalisha jambo zuri kwa Taifa,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hiyo ya Zitto imekuja baada ya kupita siku chache kwa viongozi wa Ukawa kutoa tamko la kuitaka NEC kuahirisha uchaguzi wa marudio wa ubunge katika majimbo matatu na udiwani wa kata sita uliopangwa kufanyika Januari 13, ili kuruhusu majadaliano.

Viongozi hao wa Ukawa, wakiongozwa na Mbowe walisema majadialiano hayo yatalenga kujadili kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa marudio katika kata 43, vinginevyo hawashiriki uchaguzi wa Januari.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top