Loading...
DEMOKRASIA INA GHARAMA ZAKE
Kwa mujibu wa Wikipedia wameelezea vyema asili na maana ya demokrasia. “Demokrasia (kutoka neno la Kigiriki δημοκρατία, dēmokratía, maana yake utawala wa watu: δῆμος, dêmos, maana yake "watu" na κράτος, krátos, maana yake "utawala") ni aina ya serikali. Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile sheria na katika chaguzi. Wakati mwingine huwakilishwa na viongozi wao waliowachagua.”
Kwa kifupi demokrasia ni Serikali ya Watu iliyowekwa na watu kwa ajili ya Watu. Kuna aina kuu mbili za Demokrasia ambazo ni Demokrasia ya moja kwa moja (Direct Democracy) ambayo Wananchi hushiriki moja kwa moha kwenye ngazi ya maamuzi katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Aina ya Pili ni Demokrasia Shirikishi ambapo huusisha Wananchi kuchagua wawakilishi kwenye ngazi ya maamuzi kupitia sanduku la kura. Uwakilishi huo unaweza kuwa kwenye mhimili wa Bunge na Serikali.
Nchi ya Tanzania tunafuata mfumo wa Demokrasia Shirikishi ambapo Wananchi hupata fursa ya kuchagua wawakilishi wao kwenye sanduku la kura waende kwenye ngazi ya maamuzi ya Bunge na Serikali. Tanzania tumejiwekea utaratibu wa kuchagua Viongozi kwenye kila kipindi cha miaka mitano waende kuwakilisha kwenye mhimili wa Bunge na kuwa Viongozi kwenye mhimili wa Srikali.
Kitendo cha kuwapata wawakilishi ama viongozi hutumia gharama kubwa kwenye chaguzi. Si ajabu tukasikia Mabilioni yameteketea. Hiyo ndio gharama za demokrasia ambayo nchini kwetu ni kubwa zaidi kutokana na kufuata mfumo wa vyama vingi.
Naam! Vyama vingi ni gharama sana kuitendea haki. Leo hii akijiuzulu Diwani au Mbunge inabidi kufanyike uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi husika. Ndio Katiba yetu inavyotaka ivyo ambayo leo hii imezua gumzo kubwa la Watu kuhoji gharama kubwa Taifa inayoingia kufanya uchaguzi wa marudio kuziba nafasi zilizo wazi.
Kama Taifa tuna nafasi kubwa ya kuamua yafuatayo ili kukwepa gharama za uchaguzi:-
i. Wale wote wanaojiuzulu kwa kuhama vyama vyao na kujiunga na vyama vingine wahame na vyeo vyao kwenye vyama wanavyoenda. Mathalani Mtu akihama chama ahame na chama cheo chake kibaki vile vile iwe ni Uenyekiti, ujumbe, Udiwani ama Ubunge.
ii. Wale wote wanaofukuzwa uanachama kwenye vyama vyao wabaki na vyeo vyao. Kufukuzwa uanachama kusiathiri vyeo vyao.
iii. Kuongeza muda wa Serikali kukaa madarakani ili tuepuke gharama ambazo baadhi yao wanazilalamikia kwa sasa.
iv. Kwa wale wanaofariki, nafasi ikibaki wazi Yule aliyeshika nafasi ya pili apewe ushindi ili tuokoe gharama za uchaguzi.
v. Kughairisha uchaguzi mkuu ujao na gharama za uchaguzi zielekezwe kwenye utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kuliko kuishia kwenye sanduku la kura.
Kwa sasa tulipo si sahihi kupeleka lawama moja kwa moja upande mmoja. Hatuwezi kuwazuia watu kujiuzulu, hatuwezi kuzuia watu kuhama vyama, hatuwezi kusimamisha kalenda, hatuwezi kuzuia vifo ili kukwepa gharama za uchaguzi. Ni uamuzi wetu kuamua njia sahihi tuitakayo, kwa sasa hatuwezi kukwepa gharama za demokrasia. Demokrasia ina gharama zake.
*Na Shilatu E.J*
Januari 25, 2018
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
-
Hatuna huruma, tunabeba vyote-Dk. Biteko14 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment