Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mawaziri Wa Fedha Na Mipango Wa Tanzania Na Rwanda Wakutana Kujadili Mradi Wa Ujenzi Wa Reli Ya Isaka- Kigali

Benny Mwaipaja, WFM
Mawaziri wa Fedha na Mipango wa  Tanzania na Rwanda wamekutana  Jijini Dar es Salaam kujadili namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.

Katika Mkutano huo wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili  na kufanya maboresho na pia kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.

Kikao hicho ambacho ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na wajumbe wengine.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw. Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.

Ikumbukwe kuwa mapema mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top