Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mdeme ameagiza kukamatwa mara moja na kufikishwa mahakamani wafanyakazi wote wa kitengo cha hifadhi ya chakula cha taifa NFRA kanda ya Songea waliotajwa kuhusika na utoroshwaji wa mahindi ya serikali zaidi ya gunia 1000 na kuyahifadhi kwenye ghala la mfanyabiashara binafsi kinyume cha sheria.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Ruvuma chini ya mkuu wa mkoa Christina Mdeme walifanya ziara ya kushitukiza baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna mahindi yaliyowekwa kwenye magunia ya serikali yanashushwa na kupekiwa upya kwenye mifuko ya kawaida nyakati za usiku na kuyahifadhi kwenye ghala la mfanyabiashara binafsi aliyefahamika kwa jina la Lotary Nkondola Safina.
Walinzi wa godauni hilo wamesema kuwa walipigiwa simu na mmiliki wa ghala kuwa kuna mahindi yanaletwa ya NFRA hivyo wasiondoke ambayo yametoka kituo cha Mgazini Peramiho na mengine makao makuu ya NFRA Songea magari manne yalihusika kubeba mahindi hayo Semtrela mbili na fuso mbili.
Meneja wa kitengo cha hifadhi ya chakula cha taifa NFRA kanda ya Songea Amos Mtafya amesema mara kadhaa wanatumia godauni hilo kuhifadhia mahindi ya serikali kutokana na uhaba wa maghala ya serikali.
Kufuatia hali hiyo mkuu wa mkoa alitoa amri ya kutaifisha mahindi yote yaliyokuwemo kwenye ghala hilo na kuwa mali ya serikali pamoja na kukamatwa kwa wahusika meneja wa NFRA Amos Mtafya,mtunza maghala Mariamu Mpangala na mhasibu Lugano Moses,wengine ni wafanyakazi wa godauni Beda Kinyero,mmiliki wa godauni Lotary Nkondora,Yodan Nchimbi na mlinzi Ado Ntuka.

on Friday, January 26, 2018
Post a Comment