Loading...
UVCCM yala sahani moja na Wanaoshindwa kumsaidia Rais Magufuli
Tabora 01/01/2018
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umesema wananchi wanaopata bahati wabunge wao kupewa majukumu mengine ya kiserikali viongozi wa Chama na Serikali wana dhima ya kumsaidia na kufanya kazi za kuwatumikia wananchi.
Pia umoja huo umeeleza kiongozi anayemtegea kazi mwenzake asifikiri anamkomoa mbunge, Mwakilishi, Diwani , Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa bali anakihujumu Chama cha Mapinduzi.
Matamshi hayo yametamkwa leo na Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Ndg. Kheri James alipozungumza na wananchi katika mkutano wa ndani kwenye kijiji Nkiniziwa katika Halmashauri ya.Nzega vijijini mkoani hapa .
Alisema lengo la Chama kuisimamia serikali ni kutaka kuendeleza msingi wa chama kuaminiwa na wananchi ili Ccm iendelee kubaki madarakani kwa ridhaa kutokana na kuwajali na kuwatumikia wananchi.
"Tunatakiwa kufanya kazi kwa nguvu moja ili kuendelea kuaminiwa na wananchi .Haiwezekani Rais akose usingizi kwa kuwafikiria wananchi huku ishindikane Madiwani, Wabunge ,Wakuu wa Wilaya na Mikoa washindwe kutatua kero za wananchi vijijini "Alisema Kheri
Aidha alisema iwapo viongozi wa chama na serikali hawatashughulikia shida na matatizo ya vijana pamoja na kuyapatia ufumbuzi kwa wakati huu , siku moja wanaweza kutukataa wakati tutakapowahitaji.
"Heshima yetu inatokana na kuaminiwa kwa ccm kuendelea kushika dola.Hutaweza kubaki na heshima hii ikiwa tutakosa madaraka. Bila kushika madaraka hadhi yetu itavunjika na hayupo atakaetuheshimu "Alisema.Kheri .
Alisema ikitokea kiongozi mmoja kuteleza au kukosea kwa bahati mbaya ni wajibu kwa viongozi wengine kumwita, kukaa naye pamoja kujadiliana naye na kumsahihisha kuliko kuishi bila mashirikiano na kuwekeana vinyongo.
"Nguvu ya chama chetu ni watu .Watu wenyewe ni hawa masikini, wanyonge, wakulima na Wafanyakazi. Tusipohangaika na matatizo yao na kuwatatulia watatupuuza, wakituupuuza tutapoteza heshima yetu na chama hakiko tayari hilo litokee' Alisisitiza Kheri
Katika msafara huo Kheri amefuatana na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Ndg. Tabia Mwita, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg. Shaka Hamdu Shaka , Kaimu Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg. Jokate Mwegelo na kaimu katibu Idara ya oganaizesheni, siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Mohamed Abdallah.
Kheri amemaliza ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na wanachama wa Ccm na jumuiya zake kwenye mkoa wa Tabora na kesho kupokelewa mkoan Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba.
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
-
THBUB YACHUNGUZA MAUAJI YA KIUNGONI, PEMBA8 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment