Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA VITUO VYA AFYA NCHINI

Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.  John Pombe Magufuli kwa ujenzi wa vituo  vya afya 208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.

Wameyasema hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kukagua  maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Wananchi hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini  kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas Mkomwa  ameishukuru Serikali kwa kutoa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara,  Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia maiti.

Amesema huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.

“Kwa mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa.

Naye Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vituo vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema kuwa awali kituo hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi kuhudumia wananchi lakini kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia kuondoa kero za utoaji wa Huduma za afya katika Halamashauri hiyo.

Amesema kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo kutasaidia kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma bora za afya.

Naye Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza Kamati ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na Makole.
 
Majengo ya Upasuaji na wodi ya Wazazi iliyojengwa katika kituo cha afya cha Mlali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma.
 Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe  akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu      ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top