Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa, Polepole amvaa Zitto Kabwe, Nape Naye Atia Neno


Baada ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko madogo katika Wizara kadhaa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuachwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe wameanza kuvutana mitandaoni kuhusu kuachwa kwa Mwigulu.

Kupitia mtandao wa wa Twitter Zitto Kabwe amemkaribisha, Dkt. Nchemba kwa kumwambia sasa ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi na kwamba msimamo wake ndiyo uliomponza.

"Ndugu yangu Mwigulu Nchemba karibu 'back bench' ufanye kazi ya Wananchi. Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT umekuponza. Ulikuwa msimamo madhubuti na ulisimamia haki" -  Zitto

Kufuatia kauli hiyo, Humphrey Polepole katika ukurasa wake, ameamua kumvaa Kiongozi huyo wa ACT kwa kumuita mzee wa kurukia treni kwa mbele  na kwamba Rais amefanya mabadiliko kutokana na dhamana aliyopewa na Katiba na si vinginevyo na kumtaka asipotoshe watu.

Polepole ameandika "Mzee wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo vya kilozi? Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa Kikatiba".

"Sisi tuliohudumu kwenye Serikali na Chama tunajua na kuheshimu. Usijitaftize huruma kwa mtu. Acha kupotosha hiyo si siasa safi. SAD! " Polepole

Kwa upande wa Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amemkaribisha kiongozi huyo na kumtaka waungane kuwatumikia wananchi.

"Cde Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie waliotupa kura!" Nape.


Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top