Jafo ametoa pongezi hizo wakati akipokea vituo vya afya 38, magari ya wagonjwa matatu, magari ya kuratibu shughuli za afya sita , pamoja na vifaa vilivyofadhiliwa na shirika la Kimataifa la UNFPA wakishirikiana na KOICA. Katika makabidhiano hayo,Waziri Jafo amefurahishwa na usimamizi mzuri wa ujenzi wa miundombinu hiyo kupitia utaratibu wa FORCE ACCOUNT.
Jafo amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka pamoja na wabunge wa mkoa huo kwa kuwashirikisha vyema wananchi ambao wameungana na serikali yao pamoja na wadau katika kufanikisha miradi hiyo ya afya. Katika shughuli hiyo waziri Jafo amesisitiza magari hayo tisa yatumike kwaajili ya sekta ya afya na si vinginevyo.
Wakati huo huo, Waziri Jafo amefurahishwa na wananchi wa Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza kwa kujenga vizuri sana majengo yao ya kituo cha afya Malya baada ya serikali kuwapatia fedha milioni 400.
Naye mbunge wa Sumve Mhe. Ndasa aliishukuru serikali na ameiomba kuwasaidia mashine ya X-Ray kituoni hapo ili wananchi waondokane na usumbufu wa kwenda hospitali ya wilaya iliyopo Ngudu.Waziri Jafo amemaliza ziara yake ya mikoa miwili ya Simiyu na Mwanza na kuelekea wilayani Bagamoyo kwaajili ya uzinduzi wa jengo la wazazi katika hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na viongozi wengine katika uzinduzi wa vituuo vya Afya.
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa vituo vya afya
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa vituo vya afya
Viongozi mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi wa vituo vya Afya mkoa wa Simiyu.
Majengo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika la UNFPA na KOICA.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akisikiliza maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Baadhi ya vifaa vilivyopo kwenye vituo vya afya vya mkoa huo vilivyozinduliwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Sumve Richard Ndassa katika uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya wilayani Kwimba mkoa Mwanza.
Jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Malya.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akikagua ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Malya
Post a Comment