Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 katika uzinduzi wa kitabu cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk Reginald Mengi kinachoitwa, ‘I can, I must, I will’.
Wakonta alipewa fedha hizo baada ya kujinyakulia kitita cha Dola 20,000 za Marekani sawa na Sh45.6 milioni, ikiwa ni zawadi ya ushindi wa shindano la kuandika wazo la kibiashara lililotolewa na Dk Mengi.
Akizungumza katika hotuba yake, Rais Magufuli amesema alimfahamu Wakonta baada ya kusoma historia ya maisha yake kupitia vyombo vya habari.
“Kitabu cha Mzee Mengi kiwe fundisho kwetu sote, nitoe wito kwa wafanyabiashara wote msisikilize maneno ya watu wanaowakatisha tamaa, fanyeni biashara kweli kweli”
“Hata mimi Nilijua ukishakuwa Rais huwezi kukatishwa tamaa na mtu yeyote kwa sababu wewe ni Rais lakini haikuwa hivyo, nilipoingia niliyaona.
“Nina matumaini makubwa kupitia kitabu chako hiki watanzania wengi watajenga matumaini, kujiamini na mafanikio makubwa na katika hili naomba kitabu hiki ukitafasiri kwa lugha ya kiswahili ili kupata fursa ya watanzania wengi kukisoma.
“Watanzania tuache kukatishana tamaa na ninafahamu katika historia ya Mzee Mengi yapo mengi amepambana nayo ya kukatishwa tamaa” – Rais Magufuli

“Nilisoma kwamba aligongwa na gari siku ya mahafari yake, lakini hajakata tamaa hana uwezo wa kuandika kupitia mikono yake, lakini anaweza kuandika anachokifikiria kwa kutumia ulimi wake, nitamchangia Sh10 milioni iweze kumsaidia katika mawazo yake anayoyapata kutoka kwa Mwenyezi Mungu,” amesema Rais Magufuli.
Binti huyo aliyepata ulemavu baada ya ajali, amekuwa akiandika kwa kutumia ulimi wake kwani viungo vyote vya mwili havifanyi kazi.
Hata hivyo shindano hilo lililowashirikisha vijana wa Afrika, liliibua washindi wawili akiwemo Brian Mwenda kutoka nchini Kenya.
Post a Comment