Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Humphrey Polepole, amesema kuwa hakuna uhuru usio na mipaka, hivyo basi wananchi wajiwekee mazoea ya kufuata taratibu zinazowekwa ili kuwaongoza.
Polepole ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa Ripoti ya pili Twaweza kuhusiana na tafiti zake kuhusu maoni ya wananchi wa Tanzania kuhusu Ushiriki, Maandamano na Siasa kwa mwaka 2018, ambapo Polepole amesema kuwa hata yeye huwa hafanyi mikutano ya kisiasa kwa kuwa imezuiwa hivyo anavyotembelea mikoani hufanya vikao vya ndani.
“Duniani kote hata mbinguni hakuna uhuru holela, uhuru una mipaka yake, na ndio mana ukitaka kuoa au kuolewa lazima muwe jinsia tofauti ingawa zipo nyingine watu wanaoana Jinsia moja”, amesema Polepole.
Kulingana na ripoti ya Twaweza inadai kuwa uhuru wa kutoa maoni kwa wananchi umepungua tofauti na miaka mitatu iliyopita, huku msaada wa demokrasia ya wingi unaendelea kuwa na nguvu ambapo zaidi ya asilimia 84% wanapendekeza mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Post a Comment