Lord Eyez (kulia) akiwa na wakili wake wakati wakiongea na waandishi wa habari |
Mweusi toka A- City, Lord Eyez amekutana na waandishi
wa habari akiwa na wakili wake ili kuzungumzia kesi inayomkabiri ya wizi wa
vifaa vya gari ambayo ili-make headlines sana siku kadhaa
zilizopita.
Lord eyez amesema yeye kwa sasa anaiachia mahakama
ambayo ndiyo itaweza kuchukua maamuzi ya kisheria kama yeye alihusika ama
hakuhusika katika wizi huo wa vifaa vya gari.
Wakili wa msanii huyo anayejulikana kwa jina la Peter
Kibatala amesema kesi hii imefanya mpaka Lord Eyez kuonekana kwamba yeye ndiye
mhusika wa wizi wa vifaa hivyo lakini kwa sasa hivi wanaiachia kwanza mahakama
ndiyo itakayoweza kuchukua uamuzi sahihi kuhusiana na kesi
hiyo.
Hizi kauli za mweusi huyu na wakili wake zinaonekana
zimepimwa na ruler ya kisheria kwa sababu ni kosa kisheria kujadili kesi ambayo
iko mahakamani (commenting on a pending case).
Weusi nao walisema ‘neno’ kuhusu tuhuma zinazomkabili
member huyo na kwamba tukio hili limewaathili hasa pale wanapokutana na watu
mbalimbali na kusikia story toka kwa watu kwamba wote watakuwa wanahusika katika
tukio hilo wakati ni story ambazo sio za kweli.
Kesi hiyo inatarajiwa kusomwa katika mahakama ya
mwanzo jijini Dar es Salaam tarehe 13, 14 na 15 mwezi huu wa
Novemba.
Hata hivyo the N2N soldier amesema kwa sasa anachotaka
kufanya ni kudondonsha ngoma yake mpya kali ambayo anataka kufanya ‘surprise’
kwa mashabiki wake katika industry ya muziki wa Bongo.
Lord eyez alituhumiwa na msanii mwenzake Ommy Dimpoz
kuwa alishirikiana na wenzake kumuibia vifaa vya gari lake na tuhuma hizo nzito
ambazo ni pigo kwa kundi la weusi kiujumla zilipelekea Lord Eyez kukamatwa na
kushikiliwa kwa na jeshi la polisi kwa siku kadhaa na baadae kufunguliwa kesi
mahakamani ambapo alipewa dhamana.
Post a Comment