Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya
Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa
(Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
jijini dar es salaam usiku huu ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na
taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo
wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri wa Afya na Ustawi wa
jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti
hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant
Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango
wake katika kupambana na Malaria nchini.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali
wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi
wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar
es Salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa
"Malaria Safe Companys" , kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Raymond Mushi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Rais Washirikisho la Mpira
wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt
Regency Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa
wa Malaria, kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein
Mwinyi.
Wadau waliohudhuria katika
uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka kulia ni
Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari, Vijana , Michezo na Utamaduni Bw.
Leonald Thadeo, Assah Mwmbene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa
Jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant
Mzindakaya.
Wadau mbalimbali wakiwa katika
uzinduzi huo katika Hyatt Regency Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw.
Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar
es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria
katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda
akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga
makofi katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim
Mohamed Abeid Bakhressa akitoa ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika
viwanda vyao.
Rais wa Shirikisho la mpira wa
miguu nchini TFF Bw, Leodger Tenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo
jinsi sekta ya michezo ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa
pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu
kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Meneja Mkuu wa Bodi ya Utalii
nchini Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa katika hafla hiyo, Bodi ya Utalii
nchini TTB ni moja ya taasisi zilizotambuliwa na Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda
katkatika hfla hiyo kwa juhudi zake za kupamana na ugonjwa wa
malaria.
Post a Comment