Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA ANAZIDI KUWAPA VIWEWE WANASIASA



Na Emmanuel J. Shilatu

 Mwaka huu wa 2012 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi kwa Chama Cha Mapinduzi ambapo chaguzi zimefanyika kwenye ngazi mbalimbali kuanzia ngazi za shina hadi ngazi ya Taifa.

Kwa mara nyingine tena, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeandika historia mpya baada ya kufanya mabadiliko mazito katika safu yake ya uongozi wa kitaifa.

Ni mabadiliko mazito si kwa sababu tu yamefanywa na CCM ambayo imekuwa na rekodi ya kubadili sura za watendaji wake kwa namna na kwa njia tofauti, bali kutokana na ukweli kwamba safari hii mabadiliko hayo yamehusisha watu wazito, wenye historia ya kipekee katika medani ya uongozi ndani na nje ya chama hicho.

Naam!! Huo ndio ukweli wenyewe na kwa kulithibitisha hilo angalia Wasifu mzito na historia za kutukuka za baadhi ya wateule wanaounda timu ‘mpya’ ya viongozi watendaji wa CCM, utakubaliana name kuwa safari hii Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alizichanga vyema karata zake kwa kujaza “mali” tupu!

Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji. Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Ujio wa Philip Mangula na ujio haswaa wa Mwanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM unaonekana dhahiri kuwapa viwewe, presha, matumbo joto Wanasiasa waliokuwa na ndoto za kuona anguko la CCM ama kuliona kaburi la CCM.

Kinana anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Kinana anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995.

 

Tangu wajue kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni Abdulrahaman Kinana wameshaanza kuonyesha udhaifu wao kupitia kauli na matendo yao. Kama ulisahau, naomba nikukumbushe kidogo tu baadhi ya kauli za Wanasiasa wetu zilivyojaa utata na ukiwewe wa hali ya juu.

Kama utakumbuka ilikuwa ni saa chache tu baada ya Sekretarieti mpya ya Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) kuteuliwa mjini Dodoma, aliibuka Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Wilbroad Slaa na kusema kuwa haiwezi kupambana na ufisadi wala kutekeleza dhana ya “kujivua gamba” kwa sababu wajumbe wake wenine ni sehemu ya Watuhumiwa wa ufisadi.

“ukiwachunguza viongozi hao mmoja mmoja utabaini ya kwamba kila mmoja ana matatizo yake ya kutuhumiwa katika jambo moja ama jingine na katika mazingira hayo hakuna matumaini ya mabadiliko”, alisema Dkt. Slaa

Yakapita masaa kadhaa akaibuka tena porojo zingine dhidi ya Kinana na Sekretarieti na kusema kuwa CCM ya sasa si lolote, si chochote na wala hatawaweza.

Kama haitoshi Dk. Willibrod Slaa, wakati akifungua rasmi Baraza la Mashauriano la Mkoa wa Kagera ambalo linaundwa na viongozi kutoka katika kila jimbo la mkoa huo, linalofanyika kwa muda wa siku tatu katika wilaya ya Karagwe.

Dk. Slaa alisema CHADEMA waliwezesha kufutwa kwa kodi za manyanyaso katika wilaya ya Karatu baada ya kulikalia kidete suala hilo, na ndipo CCM ilitumia sera hiyo na kuondoa kodi za namna hiyo takriban nchi nzima.

Aliongeza kuwa walianzisha pia sera ya kujenga zahanati kila kata wilayani Karatu, ambayo nayo CCM baadaye ilichukua na kisha kutangaza kuanzisha utaratibu wa kujenga zahanati kila kata nchi nzima.

“Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010, CHADEMA tuliahidi sera ya kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi nchi nzima kama tungeingia madarakani. Wakati huo CCM ilidai haiwezekani ila sasa nao wametangaza kupunguza gharama za bidhaa hizo,” alisema.

Alifafanua ni wazi kuwa CCM ikiweza kutekeleza sera ya CHADEMA ya kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi na kutoa elimu bure kabla ya mwaka 2015, watafurahi maana hawana wivu, lakini wakishindwa itakuwa ndiyo njia yao ya kuondoka madarakani.

Yote kwa yote, hayo maneno ni uthibitisho tosha kwamba maneno yote hayo yanamtokea kwa sababu hakutarajia kabisa katika maisha yake kukumbana na changamoto ya uwepo wa viongozi bora na imara, mithili ya Kinana.

Hata hivyo haitakaa itokee kwa Dkt. Slaa kuzungumzia mema ya CCM kwani alishazoea mteremko wa kisiasa kupitia siasa chafu na zisizo na staha na ndiyo maana wanalazimika kusema chochote, wakati wowote na mahali popote ili kujifariji na ujio wa kimbunga wa Kinana na Mangula.

Dai la kwanza la Dkt. Slaa ni la kumtuhumu Kinana kuwa atashindwa kutekeleza adhma mpya ya kujivua gamba kwani wote ni wale wale.

Binafsi, sioni sababu ya na hata umuhimu wa kuizungumzia kwa kirefu dhana nzima ya kujivua gamba kwa sababu inawahusu CCM pekee kwani Dkt. Slaa ameing’ang’ania kwani alidhani ililenga timua timua ndani ya chama ingewanufaisha wao (CHADEMA) kwani wangepokea makapi ambayo CCM wameyatosa.

Yeye Dokta Slaa anaukomalia ufisadi kwa nyakati zote pasipo kujitambua hata naye ni fisadi pia kwani uzinzi anaoufanya (wa kupora mke wa mtu) ni sehemu ya ufisadi anayepaswa kujivua gamba.

Dkt. Slaa anapaswa kujiuzulu kama alivyojiuzulu Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi aliyefanya hivyo kwa kushiriki ngono na makahaba nje ya ndoa.

Kabla ya kuona suala la kujivua gamba ndani ya CCM alipaswa kwanza ajiuzulu kama alivyofanya aliyekuwa  Mkurugenzi mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani (CIA), Jenerali David Patreaus (60) kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari, Paula Broadwell.

Badala ya Dkt Slaa kujiuzulu anashindwa kufanya hivyo na kuishia kuweweseka tu na kiwewe kimezidi kumpanda zidi kutokana na ujio wa Mwanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM anyemfahamu vyema na anahofu kumalizwa kisiasa.

Dk. Willibrod Slaa hatakiwi kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko walivyokuwa ‘utopia’Mzee Makamba na Mzee Mukama wanaoamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1992 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Ndugu zangu, msuko mpya wa safu ya wakuu wa idara za CCM uliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete ukiwajumuisha wanasiasa wasiojua mizaha wawapo kazini kama alivyo Philip Mangula, au makada wa muda mrefu wa chama hicho wa kariba ya Muhammad Seif Khatib na Zakia Meghji  Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulhaman Kinana umekuja kubadilisha upepo wote wa kiutendaji kazi kwa viongozi wa CCM na serikali kwa ujumla.

Mara baada ya kukabidhiwa rasmi kofia ya Ukatibu Mkuu, Kinana alihaidi kufanya kazi ya kukisafisha na kukijenga chama upya na sasa anatekeleza kwa vitendo ambapo ameanza kwa kufanya ziara kwenye mikoani na kwenda kukijenga chama.

Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia kuona viongozi wakuu wa kitaifa wakienda kufanya ziara majukwaani, mikoani na kikubwa zaidi ameshuka chini zaidi kwa kutembela mashina na matawi jambo ambalo waliomtangulia walishindwa kufanya hivyo ila Kinana ameweza.

Kwa mara ya kwanza tangu enzi za Mwalimu zikatike tumeshuhudia chama kama chama kikijipambanua kidhahiri kwa jamii nje ya serikali yake kuwa wapo tayari kuwasaidia na kuwatatulia shida zao. Tumeshuhudia huko Geita, Kinana akiwapatia leseni ya uchimbaji wa madini wachimbaji wadogo wadogo ili nao wanufaike na madini yanayowazunguka na si matajiri pekee. Huyo ndiye Kinana, Kiongozi na mtumishi mahiri asiyekaukiwa ubunifu na utendaji kazi kwa vitendo zaidi!

 

Shukrani za kipekee kwa Absalom Kibanda. Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu Na. 0717 488 622 au kupitia www.ndgshilatu.blogspot.com

 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top