Rais wa
Malawi,Joyce Banda
ZAIDI ya makahaba
2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na
kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea
juzi.
Kundi hilo
linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa
ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa
Afrika ambapo biashara ya ukahaba inaharamishwa.
“Muda wa kujadili
kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama
vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na
afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu,
Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao
ni makahaba.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.
Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.
Miaka mitatu
iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na Polisi na kulazimishw akupimwa Virusi vua
Ukimwi (VVU) na wote kukutwa wakiwa wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani
kwa kufanya biashara ya ngono huku wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza,
ambapo walichajiwa Dola7 kila mmoja na kuachiwa huru.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.
Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.
Wataalamu wa afya
nchini humo wanasema maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa makahaba hao yanafikia
asilimia 70.
Mawakili wao wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi hayo.
Mawakili wao wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi hayo.
Post a Comment