Rais Francois
Hollande wa Ufaransa amesema Ufaransa haitaingilia kijeshi mgogoro wa Mali,
lakini kama nchi za Afrika zitafanya operesheni ya kijeshi dhidi ya makundi
yenye siasa kali kaskazini mwa Mali, Ufaransa itaziunga mkono.
Rais Hollande siku hiyo alipohojiwa na vyombo vya habari vya Ufaransa alisema, hivi sasa Afrika inakabiliwa na hatari kubwa mbaliambali hasa msukosuko wa Mali, na Ufaransa inapaswa kubeba majukumu ya kuziunga mkono nchi za Afrika.
Lakini Ufaransa haitaingilia kijeshi moja kwa moja nchini Mali, na uingiliaji huo utaamuliwa na nchi za Afrika zenyewe.
Siku hiyo pia waziri wa ulinzi wa Ufaransa Bw Jean - Yves Rod Lyon amesema baadhi ya makundi la siasa kali yanaifanya sehemu ya Sahel ikiwemo eneo la kaskazini la Mali iwe maficho ya magaidi.
Kama Ufaransa na Umoja wa Ulaya hazitachukua hatua, makundi yenye siasa kali katika sehemu hiyo yatatishia usalama wa Ufaransa na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.
Jumuiya ya uchumi wa nchi za Afrika Magharibi ECOWAS jana imeitisha mkutano maalumu wa wakuu, suala la msukosuko wa Mali ni ajenda muhimu ya mkutano huo.

Post a Comment