Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati alipowasili katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na maaofisa wa Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii World Treavel Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza utalii wa Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo hufanyika kila mwaka eneo la Excel jijini London.
Balozi Khamis Kagasheki
aliitaka Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi zaidi ili kuleta mafanikio
zaidi katika maonyesho hayo na menine na kuongeza idadi ya watalii kufiki
milioni moja kwa mwaka, Tanzania ikijipanga vizuri na kutangza vivutio vyake
zaidi duniani inaweza kupata mafanikio zaidi katika utalii na kuongeza
zaidimapato yake ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii. PICHA
NA WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika hafla hiyo
ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na
makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa maandalizi mazuri katika
ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia changamoto na kuzifanyia kazi ili
kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania katika maonyesho yajayo na mengine
yanayoweza kufanyika katika nchi zingine, kulia katika picha ni Balozi Peter
Kallaghe na kulia ni Mama Balozi
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe akizungumza katika hafla hiyo
kulia ni Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na Utalii.
Baadhi
ya maofisa waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Wegoro kutoka
Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha , Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB), Balozi mdogo wa Tanzania nchini Uingereza Mh.
Kilumanga na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania ubalozini Bw.
Kashangwa.
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena wa pili kutoka kushoto akiwa
pamoja na maofisa kutoka TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Zanzibar
wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki hayupo
pichani wakati alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo.
Maofisa mbalimbali wakiingia katika hafla hiyo ya
chakula cha jioni.
Maofisa kutoka TANAPA na Ngorongoro wakiwa katika
hafla hiyo.
Ofisa
Habari wa TANAPA Bw. Shelutete kulia akiwa na Maofisa wa Kituo cha biashari cha
Tanzania nchini Uingereza katikati ni Dilunga na kushoto ni
Mohamed
Maofisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza
wakiwa katika hafla hiyo.
Wadau
wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonyesho hayo
kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw, Geofrey
Meena, Mdau Angela Msangi kutoka Shirika la Utangazaji TBC, Juma Mabakila kutoka
Jambo Concerpt na Mama Juma Pinto
Mdau
Hafsa Omary kulia akiwa na wadau wengine watanzania wanaoishi nchini Uingereza
ambao walihudumu katika banda la Tanzania wakati wote wa maonyesho
hayo.
Mkurugenzi wa
Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza mara baada ya
kufungwa kwa maonyesho hayo yaliomaliziki mwishoni mwa wiki, aliyeshika kinasa
sauti ni Hafsa Omary aliyewahi kufanya mazoezi ya mafunzo ya uadhishi wa habari
TBC hapa akikumbushia enzi zake.
Mh.
James Lembeli Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Maliasili, Utalii na Ardhi
akitoa machache mara baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo wakati akihojiwa na
Shirika la Utangazaji la Taifa TBC nchini Uingereza, ambapo aliiomba bodi ya
utalii kufanya jitihada za maksudi kuwahamasisha na kuongeza idadi ya washiriki
wazawa wa Tanzania katika maonyesho hayo
Nami nikapata
japo picha moja na mdau Hafsa Omary mara baada ya kukamizika kwa kazi nzima ya
kuripoti matukio ya maonyesho hayo yaliyomaliziki mwishoni mwa wiki iliyopita
jijini London nchini Uingereza.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kulia akimsikiliza Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Ardhi wakati alipokuwa
kichangia mazungumzo katika hafla ya chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa
maonyesho ya WTM nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita, katikati ni
Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Peter Kallaghe.
Post a Comment