![]() |
| Kocha Muingereza Stewart Hall akivishwa mataji baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo |
![]() |
| Kocha Muingereza Stewart Hall akipozi kwa picha baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo |
![]() |
| Mashabiki wa Azam wakipiga ngoma na kupuliza vuvuzela wakati wa mapokezi ya kocha Muingereza Stewart Hall kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa leo |
KOCHA Muingereza Stewart
Hall ametua jijini Dar es Salaam usiku Huku akiitaka Azam kushinda kila mechi
baada ya kurejea kuifundisha timu hiyo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya
pili.
Hall amerejea katika klabu
yake ya zamani ya Azam baada klabu aliyokuwa akiifundisha Sofapaka ya Kenya
inayomilikiwa na tajiri kukiri kwamba haiwezi kupambana na kampuni kubwa ya Azam
ambayo imeahidi kumpa mshahara mara mbili ya waliokuwa wakimlipa Wakenya
hao.
Mashabiki waliokuwa
uwanjani hapo wakipuliza mavuvuzela na kupiga ngoma, waliimba nyimbo mbalimbali
ukiwamo uliosema "Hall amerejea, homa na presha za Simba na Yanga ziko
juu."
Baada ya kutua kocha huyo, alivishwa mataji ya
maua na viongozi wa Azam waliokuwapo kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere
kwa ajili ya kumpokea.
"Nimejisikia vizuri kwa
mapokezi haya mazuri. Naahidi kufanya mazuri. Nataka Azam ishinde kila mechi.
Mambo yataanza kesho," alisema Hall ambaye aliondoka katika klabu hiyo baada
kutofautiana na uongozi kufuatia kumchezesha winga Mrisho Ngassa katika mechi ya
fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) dhidi ya
Yanga, siku chache baada ya winga huyo kupigwa picha akiibusu logo ya jezi ya
klabu yake ya zamani ya Yanga.
Uongozi wa Azam ulisema
kwamba utafanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kesho kwa
ajili ya kumtambulisha kocha huyo aliyeifundisha kimafanikio timu hiyo kwa
kuiwezesha kumaliza ikiwa ya pili katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu
uliopita na pia kuifikisha katika fainali ya Kombe la Kagame katika msimu wake
wa kwanza kushiriki. Ilifungwa 2-0 na Yanga katika fainali ya
Kagame.
Azam iliyomtimua kocha wake
aliyemrithi Hall, Mserbia Boris Bunjak, baada ya timu kuangukia katika nafasi ya
nne ya msimamo wa ligi kuu, Leo itacheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga
inayoshika nafasi ya tatu kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
picha/maelezo
na http://straikamkali.blogspot.com/






Post a Comment