Meneja Masoko wa Amana Banki Bi. Fatuma
Mruma akizinduwa huduma ya Amana Mobile Banking.
Mkuu wa Kitengo cha Bishara Bw. Sudi
Marungu – Amana Bank. akifafanua jambokuhusiana na huduma ya Amana Mobile
Banking.
Amana Bank, Benki ya kwanza Tanzania inayofuata Sharia
kikamilifu, leo tunazindua huduma ya “Amana
Mobile”.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha
Biashara (Amana Bank) Bw. Sudi Marungu alisema Dar es salaam kuwa “ Amana
Mobile ni huduma za kibenki kwa kutumia mtandao wa internet na simu zamkononi.”
“Huduma hii inalenga kuwa rahisishia wateja wetu kufanya miamala nakupata
huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na benki yetu kwa njia ya mtandao. Lengo
la kuanzisha huduma hii nikurahisisha usimamizi wa akaunti zawateja wakati
wowote, popote walipo siku saba za wiki.”
Akizungumzia kwa ufupi juu ya huduma hii Bw. Sudi
Marungu alisema, “ Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam
nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za
kipekee ambazo zinafuata Sharia kikamilifu kwakuzingatia maadili na kwa njia
iliyowazi na kwakutumia teknolojia ya kisasa kwamanufaa ya wateja wetu
wote.”
Hata hivyo, alisema ni kwa kutumia teknolojia hii ya
kisasa Amana Bank leo hii inazindua huduma ambayo inaenda sambamba na maendeleo
yakiteknolojia duniani. Mteja wa sasa anahitaji kufikiwa na huduma za ki benki
popote pale alipo wakati wowote.
Amana Mobile itapatikana kupitia simu za mkononi na
wateja ambao wameunganishwa na mitandao yote ya simu wanaweza kutumia huduma
hii.
Wakati huduma za kibenki kupitia mtandao yaani
“Internet Banking” zinaweza kufanyika kupitia kompyuta ambazo zimeunganishwa
namtandao wa internet. Huduma hizi ni zaharaka na rahisi hivyo humuwezesha mteja
kufanya miamala ya kibenki popote alipo kwa wakati anaotaka. Amana Mobile
inalenga kutoa huduma mbalimbali za kibenki kupitia simu za
mkononi.
Kupitia Amana Mobile wateja wetu wataweza kuuliza salio
la akaunti zao, kupata taarifa fupi na taarifa kamili za akaunti zao, Kununua
muda wa maongezi kwa mitandao yote ya simu zamkononi, Kufanya malipo ya awali na
Ankara kama vile kununua LUKU, kulipa bili za
DAWASCO, Star Times, TTCL Broadband,
Uhuru one, DSTV nakadhalika. Pia Amana
Mobile inamuwezesha mteja kuomba kitabu cha hundi, kuhamisha fedha kutoka
akaunti moja kwenda nyingine ndani ya benki au kuhamisha fedha kutoka kwenye
akaunti yake kwenda kwenye akaunti yake ya simu ya mkononi kama vile
M-pesa, TigoPesa na Airtel
Money.
Kwa upande mwingine Amana Internet Banking inarahisisha
usimamizi wa akaunti za wateja wetu kwani wanaweza kufanya miamala yakibenki
popote pale walipo duniani..
Moja ya faida kubwa ya huduma hii nikwamba inatoa
urahisi wakufanya miamala ya kibenki kwa muda ambao mteja anahitaji huduma hiyo
iwe ofisini, nyumbani, safarini au hata akiwa nje ya nchi. Huduma hii
imerahisisha miamala midogo midogo ambayo hapo awali iliwalazimu wateja wetu
kufika katika matawi yetu kupata huduma sasa kupata huduma popote walipo, kwa
urahisi na haraka.
Hii ni hatua kubwa kwa Amana Bank hasa ikizingatiwa
kuwa benki ina miezi kumi tu tangu ilipoanza kutoa huduma kwa wateja.
Tunawakaribisha wote kufungua akaunti Amana Bank.
Karibuni katika ulimwengu mpya kabisa wa kibenki,
unaofuata Sharia kikamilifu.
Kwa maelezo na taarifa zaidi unaweza kupata kupitia
tovuti yetu ya www.amanabank.co.tz.




Post a Comment