Baadhi ya askari jeshi wa kundi la
M23
Mapigano ambayo
yalizuka baina ya Jeshi la FARDC na Wapiganaji wa Kundi la M23 yanatajwa
kusababisha vifo vya watu mia moja na hamsini wakiwemo wapiganaji wa waasi na
Afisa mmoja wa Jeshi.
Msemaji wa Jeshi
la FARDC Olivier Hamuli amesema wamefanikiwa kuwafurusha wapiganaji wa Kundi la
M23 na sasa hali ya utulivu imeimarishwa na amewataka wananchi kuendelea na
shughuli zao.
Mapigano hayo
yamezuka kipindi hiki ambacho Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
DRC Augustin Matata Ponyo akiwa ziarani nchini Ufaransa na amekiri wanahitaji
msaada wa nchi hiyo kurejesha amani huko Kinshasa.
Katika hatua
nyingine Msemaji wa Kisiasa wa M23 Betrand Bisimwa amejitokeza na kukanusha
madai ya wao kuwatishia maisha waandishi wa habari huko Goma.
Rwanda kupitia
kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje Louise Mushikiwabo ametoa wito wa kusitishwa kwa
mapigano hayo baina ya FARDC na M23 na kuwataka waheshimu maafikiano
yaliyotolewa na Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR.
Post a Comment