RAIS
Barack Obama wa Marekani amesema nchi yake inaunga mkono hatua ya Israeli
kujilinda yenyewe.
Matamshi hayo
ameyatoa wakati wa mazungumzo yake na Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu
yaliyofanyika kwa njia ya simu, kuhusu mgogoro wa Gaza.
Rais Obama
ameelezea pia masikitiko yake kutokana na vifo vya raia wa Israeli na
Palestina.
Ikulu ya Marekani
imesema kuwa, Netanyahu ambaye alimpigia simu Rais Obama, ametoa shukrani zake
kwa Rais Obama na kwa wananchi wa Marekani.
Viongozi hao pia
wamejadiliana kuhusu kuzuia mzozo huo kusambaa.
Obama
azungumza pia na Morsi na Erdogan
Aidha, Rais Obama
amempongeza Rais wa Misri, Mohamed Morsi kwa juhudi ya kusaidia kuituliza hali
kati ya Israeli na Gaza na kusisitiza matumaini yake ya kurejea kwa utulivu
kwenye eneo hilo.
Akizungumza na
Morsi kwa njia ya simu, Rais Obama ameelezea umuhimu wa kumaliza mashambuliano
haraka iwezekanavyo ili kuzuia maisha ya raia wasio ha hatia kupotea bila
sababu.
Waziri Mkuu wa
Misri, Hisham Kandil amesema nchi yake ipo tayari kupatanisha juu ya kusimamisha
mashambiliano kati ya Israeli na Hamas. Misri ni mshirika wa Hamas, lakini pia
imetiliana saini mkataba wa amani na Israeli mwaka 1979.
Rais wa Misri, Mohammed Morsi
Mbali na
Netanyahu na Rais Morsi, Rais Obama amezungumza pia na Waziri Mkuu wa Uturuki,
Recep Tayyip Erdogan kwa njia ya simu ambapo kwa pamoja wameelezea wasiwasi wao
kuhusu hatari zinazowakabili raia wa pande zote mbili na kuelezea nia yao ya
kutaka kumaliza ghasia hizo.
Taarifa ya Ikulu
ya Marekani imeeleza kuwa Rais Obama na Erdogan pia wamesema ghasia mpya katika
Mashariki ya Kati zinahatarisha matarajio ya amani ya kudumu katika eneo
hilo.
Mapigano
yaendelea
Mazungumzo hayo
kwa njia ya simu yamefanyika, wakati wapiganaji wa Hamas wakirusha maroketi
kwenye miji ya Jerusalem na Tel Aviv jana Ijumaa.
Israeli imesema
imezifunga barabara zote kuu kuzunguka mpaka wake na Gaza, na kulielezea eneo
hilo kama la kijeshi.
Hatua hiyo ni
ishara kwamba uvumilivu wa Israeli sasa umefikia kikomo na inajiandaa kuanzisha
mashambulizi ya kwanza ya askari wa miguu katika eneo hilo tangu mwaka 2008 na
2009.
Kiasi Wapalestina
21 na Waisraeli watatu wameuawa tangu Israeli ilipoanzisha mashambulizi siku ya
Jumatano, wakati ilipomuua mkuu wa jeshi la Hamas, Ahmed al-Jabari.
Ban
Ki-Moon azitolea wito Israeli na Hamas
Katibu Mkuu wa UN, Ban
Ki-moon.
Wakati huo huo,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amezitaka Israeli na Hamas kumaliza
mashambulizi yanayoongezeka katika Ukanda wa Gaza ili kuzuia mauaji zaidi katika
Israeli na Palestina.
Msemaji wa Umoja
wa Mataifa, Martin Nersiky amesema Ban ana wasiwasi mkubwa kuhusu kuendelea kwa
ghasia kati ya Gaza na Israeli na anahofia pia kupanda kwa gharama za maisha ya
raia.
Nersiky amesema
Ban anatarajiwa kuzuru eneo hilo hivi karibuni.
Wanadiplomasia wa
Umoja wa Mataifa wamesema kuwa Ban atazuru Israeli na Misri wiki ijayo.
Post a Comment