Silaha zilizonaswa na Jeshi.
WANAJESHI wa
Nigeria wanaendeleza operesheni kali ya kuwasaka wapiganaji wa Boko Haram katika
eneo la Maiduguri Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Wanajeshi hao
wanatumia magari ya kivita na wanapewa usaidizi zaidi na helicopta za
kijeshi.
Jeshi la Nigeria
limedai kuwa limemuua kamanda mmoja mwandamizi wa Boko Haram Ibn Saleh
Ibrahim.
Raia wa eneo hilo
wamesema kuwa idadi kubwa ya watu wameuawa kwenye operesheni hiyo.
Msemaji wa jeshi
la Nigeria amesema Ibn Saleh Ibrahim aliuawa wakati wa makabiliano makali ya
riasi wakati alipokuwa na walinzi wake sita.
Maafisa wa ulinzi
nchini Nigeria wanaamini kuwa Saleh, alihusika na mauaji ya Generali mstaafu
Mohammed Shuwa mwezi uliopita.
Kundi hilo la
Boko Haram, ambao limeua raia wengi tangu mwaka wa 2009, halijasema lolote
kuhusiana na kifo cha kamanda huyo.
Post a Comment