
Naibu Waziri wa Fedha,Mh.
Janeth Mbena akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya
Resolution katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Uzinduzi
wa Kampuni hiyo umekuja rasmi mara baada ya kupata cheti cha usajili wa kutoa
bima ya afya nchini kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi ya Bima
(TIRA).

Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya bima ya Resolution,Peter Nduati akizungumza kwenye hafla hiyo ya
uzinduzi wa Kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es
Salaam hivi karibuni,ambapo alisema kuwa Kampuni yake imejipanga kufanya
mapinduzi katika soko la Tanzania.

Menjea wa Kampuni ya
Resolution Tanzania,Oscar Osir akizungumza machache kabla ya kumkaribisha
Mkurugenzi Mtendaji kuzungumza na Wadau.

Kamishna wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora akizungumza kwenye hafla
hiyo.

Naibu Waziri wa Fedha,Mh.
Janeth Mbena (kushoto) akiwa pamoja na Mjunbe wa Bodi ya Kampuni ya
Resolution,Richard Kasesela wakati wakifuatilia kwa makini taarifa fupi
iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya
Resolution,Peter Nduati (hayupo pichani).

Baadhi ya Wadau
waliohudhulia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution
katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Naibu Waziri wa Fedha,Mh.
Janeth Mbena (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya
Kampuni ya Resolution ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Kampuni
hiyo.

Picha ya Pamoja na
Wafanyakazi wote wa Kampuni hiyo ya Resolution.


Post a Comment