

Watu watatu akiwemo mtoto mdogo
wameumizwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba kwaa jiwe
lililoporomoka kutoka mlimani jijini Mwanza.
Waliokumbwa na ajali hiyo ni Bw. Msalam Husein ambaye
ni dereva (30) na mkewe Bi. Nadia Grecian ambaye ni mama wa nyumbani (25)
pamoja na kichanga wao Asfati Mslam (aliyechini ya umri wa
mwaka).
Tukio
hilo limetokea leo hii majira ya saa 6:00 mchana katika nyumba wanayoishi kilima
cha Sabato mtaa wa Ngara eneo la Mlimani B Kirumba jijini Mwanza ambapo pamoja
na kwamba ni majira ya mchana watu hao mke na mume walikuwa wamejipumzisha
kitandani, (yawezekana kutokana na hali ya hewa kwa mvua inayoendelea kunyesha
leo tangu asubuhi hadi muda huu tunakupa taarifa) ndipo wakakutana na ajali
hiyo.
Mtoto
Asfati Mslam alifariki dunia jana majira ya saa 9 na dakika kadhaa za alasiri
katika hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure alikokimbizwa yeye na wazazi
wake mara baada ya kuumizwa vibaya kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao kupitia
mawe yaliyoporomoka kutoka kwenye msingi wa nyumba iliyo eneo la juu mlimani
jijini Mwanza. Mtoto Asfati Mslam
amezikwa kwenye makaburi ya Waislamu ya Ngara Kirumba eneo la Mlimani
B.




Post a Comment