Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya
wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa, wakati alipofika katika Kijiji cha
Ilembo Mkoa wa Katavi, Nov 24, kwa ajili ya kuzindua rasmi Ujenzi wa Nyumba za
gharama nafuu, zinazojengwa na Shirika hilo, ambapo jumla ya nyumba 250,
zinatarajia kujengwa katika eneo hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,
Nehemiah Kyando Mchechu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuashiria
uzinduzi rasmi wa ujenzi wa Nyumba za Gharama nafuu zinazojengwa na Shirika la
Nyumba la Taifa, NHC katika Kijiji cha Ilembo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo
ulifanyika Nov 24, 2012 katika kijiji hicho. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
hilo, Nehemiah Kyando Mchechu (wa pili kulia) ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Medeye na (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi,
Dkt. Rajab Lutengwe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal (wa
pili kushoto) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck
Ole Medeye (wa pili kulia) wakikagua sehemu ya ujenzi wa nyumba hizo bada ya
uzinduzi wa mpango wa Ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na Shirika
la Nyumba la Taifa NHC, katika kijiji cha Ilembo Mkoani Katavi Nov 24,
2012
Post a Comment